Michezo

Udukuzi wa mitandaoni kuinyima Uingereza uhuru kombe la dunia 2018

Timu ya taifa ya Uingereza pamoja na benchi lake la ufundi watashauriwa kutotumia mtandao wa Wi-fi  wakati wa kombe la dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Urusi hapo mwakani kwa kuhofia udukuzi.

Shirikisho la soka nchini Uingereza lina wasiwasi kwamba habari muhimu zinazo ihusu timu hiyo na maelezo mengine ya kiufundi huenda zikadukuliwa.

Hofu ya wizi wa data pia imeangaziwa kufuatia udukuzi wa mwezi uliopita uliofanywa na kundi la Fancy Bears kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku katika soka.

Fancy Bears inadai kwamba habari hizo zilizofichuliwa mnamo mwezi Agosti zinaonyesha kwamba takriban wachezaji 160 walifeli vipimo vya utumizi wa dawa za kusisimua misuli mwaka 2015, huku wakati idadi hiyo ikidaiwa kuongezeka na kufikia 200 mwaka uliofuta.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents