Michezo

UEFA: Hizi ndio takwimu kati ya manchester United Vs Barcelona kabla ya mchezo wa kesho

Unapozungumzia michuano ya klabu bingwa barani Ulaya ndio michuano yenye heshimu kwa ngazi za vilabu barani humo lakini sio ulaya tu hata kwenye mabara mengine michuano ya kvilabu katika barana zima inakuwa na mvuta sana sio tu mvuta hata pesa inakuwepo kwa hali ya juu lakini hapo ni kwenye vilabu, tukiangalia kupitia mchezaji mmoja mmoja kwao inafaida kubwa sana kwani licha ya kupata pesa kwa kushiriki michuano hiyo pia anatengeneza jina lake.

Katika michuano ya mwaka huu ambayo imefikia hatua ya robo fainali taifa la Uingereza limefanikiwa kupeleka vilabu vinne mwaka huu kwenye michuano hiyo lakini hadi hivi sasa vilabu vyote vinne vimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwa maana hiyo inawezekana mmoja ya klabu kutoka nchi hiyo au hata viwili vikafanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano hiyo mikubwa.

Vilabu ambavyo vimefanikiwa kutinga hatua hiyo ni pamoja na Juventus kutoka italia, Ajax kutoka uholanzi, Porto kutoka ureno, Barcelona kutoka Uhispania, Manchester United kutoka Uingereza, Manchester City kutoka Uingereza, Tottenham kutoka Uingereza na Liverpool kutoka Uingereza pia.

Michezo ya robo fainali itakuwa hivi:- Leo Jumanne, Liverpool vs Porto na Tottenham vs Manchester City, Kesho Manchester United vs FC Barcelona na Ajax vs Juventus

Katika mtanange unaosubiriwa kwa hamu ni kati ya Manchester United watakapowakaribisha Barcelona, Bila shaka kwa sasa Barcelona ni klabu yenye maisha ya furaha tele. Wanaongoza ligi ya Uhispania, maarufu kama La Liga, kwa wigo wa alama 11. Pia wameshatinga fainali ya Kombe la Uhispania.

Kwa vyovyote vile, miamba hiyo ya Uhispania chin ya kocha Ernesto Valverde watakuwa na kila sababu ya kujiamini pale watakapominyana na Manchester United keshokutwa Jumatano katika mchezo wa raundi ya kwanza ya robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya katika uga wa Old Trafford. Ushindi wao wa mwisho ulikuwa dhidi ya Atletico Madrid juzi Jumamosi ambapo mpaka dakika ya 84 ilikuwa hakuna bao.

Zikiwa zimesalia dakika tano tu mchezo kuisha, Luis Suarez alituma kombora moja lililomshinda mlinda mlango wa Atletico Jan Oblak ambaye alikuwa nyota kwa upande wa timu yake kwa kuokoa michomo mingi ya Barca.

Zahma tena ikarudi baada ya dakika moja tu kwa Lionel Messi kupachika bao la pili baada ya kuwahadaa walinzi na mlinda mlango wa Atletico.

Lionel Messi
Image captionLionel Messi ameshapachika mabao 33 ya La Liga mpaka sasa huku akikaribia kushinda kiatu cha dhahabu kwa msimu wa tatu mfululizo.

Matokeo dhidi ya Atletico ilikuwa ni mara ya pili kwa Suarez na Messi kuamua matokeo ya mwisho ya klabu yao ndani ya dakika za lala salama.

Jumatano wiki iliyopita, Barcelona walitoka sare ya 4-4 dhidi ya Villarreal. Mpaka dakika ya 89 Villarreal walikuwa wanaongoza kwa goli 4-2.

Ilipotimu dakika ya 90 Suarez akaandika bao la tatu, na ndani ya dakika mbili za majeruhi, Messi akaiandikia Barcelona goli la nne na kuondosha aibu ya kufungwa na timu iliyopo kwenye nafasi tatu za mkiani.

Habari mbaya zaidi kwa Manchester United ni kuwa, Suarez na Messi wamekuwa wakifumania nyavu kwa kasi msimu huu.

Wawili hao wamefunga magoli 14 katika mechi sita zilizopita (Magoli 10 Messi, Suarez manne), na kwa msimu huu mpaka sasa Messi kashafunga magoli 43 katika michezo 40. Pia ametoa pasi za mwisho 17 zilizozaa magoli.

Wachambuzi wengi wanaamini huu ndiyo unaweza ukawa msimu bora zaidi kwa Messi, na ni wale ambao hawajamwangalia akicheza kwa siku za hivi karibuni tu ndio ambao wataendelea kudhania kuwa kiwango chake kimeporomoka.

Messi na Suarez ‘wanafanya kazi’ vizuri pamoja wakiwa uwanjani, lakini si kwamba wao ndio watu hatari pekee kwenye kikosi cha Barca.

Mchezaji amabaye anashirikiana kwa karibu zaidi na Messi ni beki wa pembeni Jordi Alba, ambaye amekuwa bingwa wa kumpenyezea Messi mipira kwenye eneo la hatari.

Swali kubwa zaidi ni nani ataungana na wawili hao kwenye safu ya ushambuliaji dhidi ya Manchester United. Jumamosi waliungana na na winga wa zamani wa Liverpool, Philippe Coutinho, ambaye mashambulizi yake yote yalinaswa na kipa wa Atletico.

Coutinho hta hivyo hajakuwa na msimu mzuri sana mpaka sasa, na kuna uwezekano mkubwa nafasi yake ikachukuliwa na Ousmane Dembele iwapo atakuwa ameimarika kiafya.

Gerard Pique
Image captionGerard Pique ameendelea kuwa na msimu mzuri baada ya kubwaga manyanga kuchezea timu ya taifa.

Kocha Valverde pia ana ‘uti wa mgongo’ imara unaoongozwa na kipa Marc-Andre ter Stegen, beki wa kati kisiki Gerard Piquena kiungo Arthur Melo.

Arthur ndiye mchezaji ambaye mashabiki wengi wa Man United hawamfahamu, ni raia wa Brazil aliyejiunga na miamba hiyo ya Uhispania akitokea klabu ya Gremio mwanzoni mwa msimu.

Lakini hata kama hujawahi kumuona kabla, anaweza asiwe mgeni sana machoni mwako maana aina yake ya uchezaji ni kama nguli Xavi.

Japo ni jambo gumu kumlinganisha mtu yeyote na Xavi. Arthur amekuwa akicheza vizuri kwenye kiungo cha kati na kuwa na wastani wa takwimu mzuri kama Xavi.

Katika mechi ya raundi ya kwanza na Valencia mwanzoni mwa msimu, kiungo huyo mwenye miaka 22 alifikia rekodi ya kupiga pasi nyingi zaidi (135) kwenye mchezo wa ugenini wa La Liga. Rekodi kama hiyo iliwekwa mwaka 2012 na Xavi.

Ole Gunnar Solskjaer
Image captionKocha wa Barcelona Ole Gunnar Solskjaer alienda kushuhudia mchezo kati ya Barcelona na Atletico mwishoni mwa wiki.

Licha ya kuwa na mafanikio mazuri nyumbani, kwa sasa Klabu Bingwa Ulaya ndiyo kipaumbele namba moja kwa kalabu hiyo.

Miamba hiyo imekuwa ikiyaaga mashindano hayo katika hatua ya robo fainali kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita.

Katika kipindi chote hicho, habari mbaya zaid kwa Barcelona ilikuwa ni, mahasimu wao wa jadi, klabu ya Real Madrid ndiyo ilikuwa ikinyanyua ndoo.

Tayari Messi ameshawaahidi mashabiki wa Barcelona mwanzoni mwa msimu huu kuwa: “Tunaahidi kuwa tutafanya kila tuliwezalo ili kulirudisha kombe lile zuri hapa Camp Nou.”

Lakini Manchester United hawatakiwi kukata tamaa kabisa, sababu Barcelona wanafungika.

Udhaifu mkubwa wa Barcelona ni safu yake ya ulinzi, ambayo kwa mara kadhaa imedhihirisha kuwa haiwezi kuzuia mashambulizi ya kushtukiza. Hilo lilionekana wazi kwenye sare yao ya 4-4 na Villarreal ambao wanambana ili kujinusuru na kushuka daraja.

Barca pia kwa miaka ya hivi karibuni hawana rekodi safi katika mechi za ugenini katika hatua ya mtoano kwenye kombe la Klabu Bingwa.

Barca hawajashinda mechi yoyote kwenye hatua ya mtoano toka walipoifunga Arsenal 2-0 Februari 2016 – na kwenye kipindi hicho wamepokea vipigo vizito ugenini kutoka kwa Atletico (2-0), Paris St Germain (4-0), Juventus (3-0) na Roma (3-0).

Hivyo, kuna kila sababu kwa United kuamini kuwa wanaweza kuiadhibu Barcelona inayoongozwa kikamilifu na Lionel Messi, lakini haitakuwa kazi rahisi.

N ahizi ndio rekodi zao katika michuano hiyo wakiwa wamekutana mara 11 Manchester United akishinda mara 3 na FC Barcelona wakishinda mara 4 na sare 4:-

Manchester United Vs Barcelona

United Games won:3
Games drawn:4
Barcelona Games lost:4
DateMatchResultScoreCompetition
07 Mar 1984Barcelona v Manchester UnitedL2-0UEFA European Cup Winners Cup
21 Mar 1984Manchester United v BarcelonaW3-0UEFA European Cup Winners Cup
15 May 1991Barcelona v Manchester UnitedW1-2UEFA European Cup Winners Cup
19 Oct 1994Manchester United v BarcelonaD2-2UEFA Champions League
02 Nov 1994Barcelona v Manchester UnitedL4-0UEFA Champions League
16 Sep 1998Manchester United v BarcelonaD3-3UEFA Champions League
25 Nov 1998Barcelona v Manchester UnitedD3-3UEFA Champions League
23 Apr 2008Barcelona v Manchester UnitedD0-0UEFA Champions League
29 Apr 2008Manchester United v BarcelonaW1-0UEFA Champions League
27 May 2009Barcelona v Manchester UnitedL2-0UEFA Champions League
28 May 2011Barcelona v Manchester UnitedL3-1UEFA Champio

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents