Michezo

UEFA ilivyomtoa kafara Ng’olo Kante kwenye kikosi bora cha Ulaya kisa Cristiano Ronaldo

UEFA ilivyomtoa kafara Ng'olo Kante kwenye kikosi bora cha Ulaya kisa Cristiano Ronaldo

Imeripotiwa mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo alipata kura kidogo za mashabiki katika kundi la washambuliaji Bora wa UEFA kwa mwaka 2019 ukilinganisha na Sadio Mane, Robert Lewandowski na Lionel Messi.

Kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa Dail Mail nchini Uingereza, Shirikisho hilo la Soka barani Ulaya UEFA liliamua kubadili mfumo wa kikosi cha mwaka kilichopigiwa kura na mashabiki kwa kumtoa kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa  Ng’olo Kante na kumuweka mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo.

Kikosi bora cha UEFA mwaka 2019, Ng’olo Kante na Cristian Ronaldo

Kikosi hicho kilichopigiwa kura na mashabiki dunia nzima kilitangazwa Jumatano, Januari 15, 2020 kikiwa na mfumo wa 4-2-4, ambapo wachezaji waliotajwa katika kikosi hicho ni Golikipa: Alisson, Walinzi: Trent Alexander-Arnold, Matthijs De Ligt, Virgil Van Dijk na Andy Robertson, Viungo: Frenkie De Jong na Kevin De Bruyne pamoja na Washambuliaji: Lionel Messi, Robert Lewandowski, Cristiano Ronaldo na Sadio Mane.

Inaelezwa kuwa Ronaldo alipata kura chache dhidi ya washambuliaji wenzake, Messi, Lewandowski na Mane na wakuu wa shirikisho hilo hawakuridhishwa na Ronaldo kuachwa kwake, hivyo wakaamua kufanya mabadiliko hayo na kupelekea sintofahamu kubwa.

Inadaiwa kuwa kikosi hicho kilikuwa tayari kutangazwa tangu wiki iliyopita lakini suala la Ronaldo ndilo lililopelekea kucheleweshwa kwa taarifa hiyo kutangazwa

Lakini msemaji wa UEFA akijibu kuhusu mabadiliko hayo amesema, “mabadiliko hayo ya kumtoa Kante na kumuweka Ronaldo yamefanywa kwa kuzingatia mafanikio yake katika michuano ya ‘Nations League’ na mfumo wa kikosi cha mwaka huu umefanywa ili kuendana na kura zilizopigwa na mashabiki pamoja na mafanikio ya wachezaji katika michuano mbalimbali ya Ulaya“.

Miaka iliyopita, mashabiki walikuwa wakichagua wachezaji pamoja na mifumo, ambapo miaka mitano kati ya sita iliyopita ulitumika mfumo wa 4-3-3 na mwaka 2017 ulitumika mfumo wa 4-4-2.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents