Michezo

UEFA Super Cup: Madrid waichakaza Manchester United (+Video)

Klabu ya Real Madrid jana usiku imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Super Cup barani Ulaya kwa kuichakaza Manchester United goli 2-1.

Sergio Ramos lifts the Super Cup after Real Madrid beat Manchester United 2-1 in Macedonia
Madrid wakishangilia baada ya ushindi jana

Goli la kwanza la Real Madrid lilitupiwa na Casemiro kunako dakika ya 24 huku La pili likifungwa dakika ya 52 kipindi cha pili na Isco.

Katika Kipindi cha Pili Manchester United walianza vizuri kwa mpira wa kasi juhudi ambazo zilizaa matunda kwa kupata goli la kufuta machozi kupitia kwa Romelu Lukaku kunako dakika ya 64 na mpaka filimbi ya mwisho Manchester United 1 Madrid 2.

Fainali hiyo ambayo inakutanisha timu mbili yaani mshindi wa klabu bingwa ulaya na mshindi wa Europa League ilikuwa na mvuto wa kipekee kwa mashabiki wa soka ulimwenguni kutokana na historia ya timu hizo.

Tazama magoli yote hapa chini

https://youtu.be/tPCig1YDR_o

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents