UEFA watangaza kikosi bora cha mwaka 2017, EPL yafunikwa na La Liga

Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) leo alhamisi Januari 11 limetangaza kikosi bora cha wachezaji 11 cha mwaka 2017 ambapo kwenye kikosi hicho Ligi Kuu soka Hispania (La Liga) imeongoza kwa kutoa wachezaji 7 kwenye majina hayo.

Majina ya wachezaji waliotoka La Liga ni Lionel Messi (FC Barcelona), Cristiano Ronaldo, Toni Kroos, Luka Modrid, Sergio Ramos na Marcelo wote kutoka Real Madrid.

Wachezaji kutoka Ligi Kuu England (EPL) ni Eden Hazard (Chelsea) na Kevin De Bruyne kutoka klabu ya Manchester City.

Kutoka Italia Seria A ni Gianluigi “Gigi” Buffon na Giorgio Chiellini wote kutoka klabu ya (Juventus), huku Ligi Kuu Soka ya Ufaransa (League 1) ikitoa mchezaji mmoja Daniel Alves kutoka PSG.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW