Habari

UEFA YATISHIA KUVUNJA MECHI PAKIWEMO UBAGUZI


RAIS wa Shirikisho la Soka Ulaya, (UEFA) Michel Platini, amesema njia bora ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika mchezo wa soka ni kwa marefa kusimamisha mechi wakati inabainika ubaguzi umetoka.
Wiki iliopita kipindi cha BBC cha Panorama kilionyesha matukio ya ubaguzi wa rangi katika viwanja vya Poland na Ukraine,ambako ni kwa wenyeji wa mashindano ya mataifa bingwa barani Ulaya mwaka 2012, yanayoanza siku ya leo Ijumaa.

” Nafkiri, hiyo ndiyo njia nzuri ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika mchezo huu.”
Platini alikanusha taarifa kuwa hadhi yake itashuka kama kutatokea matukio ya ubaguzi wa rangi katika mashindano ya mwaka huu 2012.
” Hadhi yangu, kwa kuwa kuna wabaguzi wa rangi nchini Poland na Ukraine – unafanya mzaha?
” Jukumu langu ni kukabiliana na tatizo hilo – na nimejitahidi kubadilisha sheria, kubadilisha kanuni, kusaidia kwa kauli mbiu ‘ Watu wote ni sawa’ na ‘ Isifanyike Tena’. Tunawasaidia sana, tunafanya mengi kukabiliana na ubaguzi wa rangi kuhakikisha tunakomesha tabia hiyo kwenye mchezo wetu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents