Michezo

UEFAChampionsLeague: Bayern, PSG, Barcelona zang’ara, Chelsea wakibanwa mbavu darajani

Jana usiku kulikuwa na michezo nane katika viwanja tofauti tofauti barani Ulaya kwenye michuano ya Klabu bingwa ambapo tumeshuhudia klabu kubwa zikiendeleza ubabe kwenye michuano hiyo kwa ushindi mnono huku Chelsea wakilazimishwa sare ya goli 3-3 na klabu ya Roma kutoka Italia kwenye uwanja wao wa Stamford Bridge.

Chelsea hao ndio walianza kutawala mpira kwa kutangulia kufunga magoli mawili ya haraka kunako kipindi cha kwanza kupitia kwa David Luiz na Eden Hazard huku goli la kwanza la Roma likitupiwa na Aleksandar Kolarov na hadi mapumziko Chelsea 2 Roma 1.

Kipindi cha pili mambo yalienda kombo kwani mshambuliaji wa Roma, Edin Nzeko alitupia magoli mawili akiwaacha Chelsea wakihaha mpaka dakika za mwisho Eden Hazard alivyokuja kusawazisha na matokeo kubakia 3-3. Matokeo mengine kwenye kundi hilo Atletico Madrid walilazimishwa sare nao wakiwa ugenini dhidi ya Qarabag FK. Tazama msimamo wa Kundi C kwa sasa

Matokeo mengine ni klabu ya PSG ya nchini Ufaransa iliibuka na ushindi mnono wa magoli 4-0 ugenini dhidi ya Anderlecht magoli yamefungwa na Kylian Mbappe, Edinson Cavani, Neymar na Angel Di Maria.Matokeo mengine kwenye kundi hilo ni ushindi mnono wa Bayern Munich wa goli 3-0 dhidi ya Celtic. Tazama msimamo wa Kundi B baada ya matokeo ya jana usiku

Barcelona nao wakiwa nyumbani walifanikiwa kuwaadhibu Olympiacos kwa goli 3-1, magoli ya Kutoka kwa Lionel Messi, Lucas Digne na moja la kujifunga yaliwapa ushindi mnono miamba hao wa Uhispania. Matokeo mengine kwenye kundi hilo, Juventus walifanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza kwenye kundi hilo kwa kuwalaza Sporting CP goli 2-1. Huu ndio msimamo wa Kundi D baada ya matokeo ya jana

Matokeo mengine ya Kundi A, Manchester United walipata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Benfica wakiwa ugenini na Basel nao wakiwa ugenini waliiadhibu CSK Moscow goli 3-0.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents