Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

UEFAChampionsLeague: Liverpool wavutwa shati na Sevilla (+video)

Klabu ya Liverpool kutoka Uingereza jana usiku imelazimishwa sare ya goli 2-2, na klabu ya Sevilla kutoka Hispania, Kwenye michuano ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

https://youtu.be/sR7l17FxMd8

Sevilla ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Liverpool kunako dakika ya 5 kipindi cha kwanza kupitia kwa, Wissam Ben Yedder kabla ya Mohammed Salah na Firmino kuongeza goli la pili na mpaka mapumziko ilikuwa 2-1.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi kwa kasi lakini bahati haikuwa kwa Liverpool kwami mnamo dakika ya 72, mshambuliaji wa Sevilla, Joaquin Correa aliisawazishia Sevilla, mpaka dakika 90 ubao ulisomeka 2-2.

Matokeo mengine kwenye ya Kundi E, Maribor nao walilazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Spartak Moscow, matokeo ambayo yanafanya kundi hilo kila timu kuwa na alama 1.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW