Michezo

UEFAChampionsLeague: Neymar, Mbappe wababe wa vita PSG (+Video)

Jana usiku kulikuwa na michezo ya hatua ya makundi ya klabu Bingwa barani Ulaya, ambapo tulishuhudia klabu ya PSG ikionesha makali yake kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo kwa msimu huu kwa kuichapa Celtic goli 5-0 ugenini.

https://youtu.be/U4vQLPqmT4I

Hakuna ubishi wowote kwamba PSG kwa sasa ni moja ya klabu za kuogopwa zaidi hii ni kutokana na safu yake ya ushambuliaji, ambayo inaongozwa na Neymar Jr, Mbappe na Cavan ambao wote kwenye mchezo wa jana walitupia.

Neymar alikuwa wa kwanza kufungua akaunti ya magoli, na baadae Mbappe akaongeza moja kisha mkongwe Cavan akatupia goli mbili huku beki wa Celtic, Mikael Lusting akijifunga mwenyewe kwenye jitihada za kuokoa.

Matokeo mengine kwenye kundi hilo ni Bayern Munich wameibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Anderlecht.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents