Michezo

UEFAChampionsLeague: PSG waangamizwa Ujerumani, Man United yafanya kweli

By  | 

Jana usiku kulikuwa na michezo ya klabu bingwa barani Ulaya ambapo Matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris Saint Germain ilikubali kichapo cha goli 3-1 dhidi ya mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich.

Magoli ya Bayern Munich yamefungwa na Robert Lewandowski, na magoli mawili ya Corentin Tolisso huku goli la kufutia machozi la PSG likifungwa na Kylian Mbappe.

Matokeo mengine ni wababe wa Uingereza Manchester United wameibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya klabu ya CSKA Moscow.

Kwa matokeo hayo Klabu ya PSG, Bayern Munich, Manchester United, FC Basel, FC Barcelona, Juventus, Roma, Chelsea, tayari zimeshafuzu kuingia kwenye hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Tazama matokeo mengine ya jana usiku:

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments