Technology

Ufahamu mfumo mpya wa wanafunzi kujisomea bure wakiwa nyumbani kuepuka Corona – Video

Ufahamu mfumo mpya wa wanafunzi kujisomea bure wakiwa nyumbani kuepuka Corona - Video

Wakati mamilioni ya wanafunzi wakiwa nyumbani ili kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona, Shulesoft imeiunga mkono serikali kwa kujitolea kuja na programu ambayo itawafanya wanafunzi kuendelea kufuatia masomo yao kwa njia ya mtandao bure.

Programi hiyo itawawezesha wanafunzi wa kuanzia darasa la awali hadi vya kidato cha sita kufuatilia vipindi kama kawaida.

ShuleSoft mpaka sasa inatumika na shule zaidi ya 300 nchini huku ikiwa na zaidi ya watumiaji 100,000 ambao hupata huduma mbalimbali ikiwemo kufuatilia Uendeshaji wa Shule, Maendeleo ya Mwanafunzi kimahudhurio, Ufaulu, kulipia Karo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Shulesoft, Ephraim Swilla alisema ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa mpangilio maalumu kutakuwa na ratiba ya masomo kwa kila darasa ili wanafunzi wajifunze na watapewa nafasi ya kuuliza maswali.

“Programu hii ni ya bure kwa kila mtu kujifunza, lakini pia mtu ambaye ataweza kuchelewa kipindi ataweza kukiona kwani kitakuwa mtandaoni na anaweza kupakua katika simu yake na kukiangalia kwa utulivu,”

“Ili mtu aweze kuhudhuria masomo hayo lazima awe na kifaa kinachomiwezesha kutumia intaneti na mpaka sasa tuna walimu zaidi ya 3000 lakini bado tunataka kutanua wigo kwa walimu waliotayari kujitolea ili tuwafikie watu wengi zaidi,” alisema

Alisema shule binafsi zinazotaka kujiunga zitajaza taarifa zao kwenye Mtandao wa shulesoft.co.tz na kuunganishwa moja kwa moja huku wanafunzi wa Shule za Serikali wakitengenezewa mfumo mmoja utakaowawezesha wote kujiunga inayofahamika jifunze.shulesoft.com.

“Wanafunzi wote watakapo ingia ndani watakutana na vipindi vitavyokua vinarushwa mubashara na walimu mbalimbali ambao watapenda kujitolea kufundisha wanafunzi na kujibu maswali yao,”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents