Burudani

Ufahamu mjengo wanaokaa washiriki wa BSS


Kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook wa Bongo Star Search, leo kumewekwa picha ya jumba la kifahari wanapokaa washiriki wa shindano hilo.

Ni jumba la kifahari ambalo limevuta hisia za wengi huku kila mmoja akiwa na la kwake la kusema.

“Hekalu la ukweliiii,halafu mwakani mnajenga jipyaaa?” amehoji mchangiaji mmoja.

“Mjengo mzurI bt washiriki wakimaliza shindano mtawaendeleza vp achana na mshind 1,2, na 3 ambao wanapata zawad! Mjipange,” aliandika mwingine.

“Jumba sawa ila linawasaidieje hao washiriki? maana mshindi akisha tangazwa akipewa na zawadi kesha ridhika na masiha, kuimba kwenyewe basi tena, na nyinyi mnaishia hapo hapo baada ya kupata faida hata ushauri tena kwa mshindi hakuna, yaani katika wasanii woote ambao wameshinda hapo kwenu, ni mmoja tu ndio namuona anafanya walau muziki ambao watu wanamuona, Ramadhani ambaye yuko Twanga,,, kwanini msibuni kitu kingine baada ya kumaliza mashindano ili kuweza kutangaza vipaji mlivyovumbua?” alishauri mchangiaji mwingine.

Mshindi wa mwaka huu wa shindano hilo ataibuka na kitita cha shilingi milioni 50.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents