Habari

Ufahamu mkasa wa kidume huyu kutoka Ethiopia, aliyekufa na kufufuka na hatimae kufa tena

Mawanamume wa Ethiopia ”aliyefufuka” wakati wa mazishi yake miezi mwili iliyopita amefariki dunia. Hirpha Negero alithibitishwa kufa mwezi Novemba ambapo aliwekwa ndani ya jeneza kwa saa tano, lakini wakati wa mazishi yake wanavijiji walisikia akigonga jeneza.

Bw.Hirpha alisimulia BBC yaliyomfika wakati huo.

”Nilisikia mtu akilia. Nilijihisi kuishiwa na pumzi ndipo nikajaribu kujitoa katika hali hiyo. Nilikua mnyonge , hata sikuweza kuzungumza.”

Baadae anasema alifanikiwa kuwaita watu, “Hapakua na mtu yeyote karibu?”

Mchimba kaburi Etana Kena anasema watu waligutushwa na tukio hilo na wote walikimbia na kuliacha jeneza, ilibidi ajifungulie mwenyewe.

Baada kisa hicho hafla ya mazishi iligeuka kuwa sherehe.

Kena ambaye pia ni mjomba wa Hirpha alisema: “Nimezika zaidi ya miili 50 au 60. Sijawahi kushuhudia maajabu kama haya. Alionekana kama amefariki.”

Bw.Hirpha alisema kuwa aliona ‘mahali pazuri sana wakati alipokua amepoteza fahamu, ambapo mwanamume aliyekua amevalia nguo nyeupe alimwambia ”rudi nyumbani”

Dkt Birra Leggese ameiambia BBC, huenda Hirpha alipoteza fahamu vibaya sana “deep coma”.

Mchimba kaburi wa awali alimzika tena Hirpha kwa mara ya pili siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kifo chake.

Alisema: “mara hii nilikua na hakika amefariki kwasababu, alishuhudia jinsi alivyougua kwa muda mrefu.”

Chanzo BB,

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents