Michezo

Ufaransa watwaa Kombe la Dunia, Kylian Mbappe aingia kwenye rekodi iliyowekwa na Pele mwaka 1958

Ufaransa watwaa Kombe la Dunia, Kylian Mbappe akiingia kwenye rekodi iliyowekwa na Pele mwaka 1958

Timu ya Taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2018 kwa kuichapa Croatia bao 4-2.

Magoli ya Ufaransa yamefungwa na Mbappe, Griezmann, Pogba na moja akijifunga Mario Mandzukic kunako dakika ya 18.

Kwa upande wa Croatia magoli yamefungwa na Ivan Perisic na Mario Mandzukic na hadi kipenga cha mwisho Ufaransa Croatia 2.

Goli la Kylian Mbappe (19) kunako dakika ya 65 limemfanya aingie kwenye rekodi ya wachezaji wadogo chini ya miaka 20 waliocheza fainali ya Kombe la Dunia na kufunga goli, rekodi ambayo ilikuwa inashikiliwa na mchezaji bora wa muda wote kutoka Brazil, Pele.

Pele akilia kwa furaha mwaka 1958

Pele akiwa na miaka (17) aliiweka rekodi hiyo mwaka 1958 wakati Brazil ilipotwaa kombe la Dunia la kwanza kwa nchi hiyo ambapo Pele alitupia goli kati ya magoli matano ambayo Brazil  iliichapa Sweden.

Kylian Mbappe

Mbappe pia ametwaa tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2018 kama alivyofanya Pele mwaka 1958.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents