Ufaransa yatinga fainali kombe la Dunia

Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Dunia baada ya kuifunga Ubelgiji bao 1 – 0.

Ufaransa imetinga hatua hiyo ya fainali baada ya kupata bao lake dakika ya 51 kupitia kwa Umtiti.

Mchezo wa pili wa nusu fainali unatarajiwa kupigwa hapo kesho baina ya timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya Croatia ambapo mshindi wa mechi hiyo atakabiliana na Ufaransa tarehe 15 siku ya Jumapili.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW