Habari

UGANDA: Aliyetoweka akiwa kidato cha pili, Arudi akiwa na miaka 24 na watoto 7

UGANDA: Aliyetoweka akiwa kidato cha pili, Arudi akiwa na miaka 24 na watoto 7

Agnes Nelima mzaliwa wa Kijiji cha Misimo, Webuye Magharibi kaunti ya Bungoma, amerejea nyumbani baada ya miaka 24, akiwa na watoto saba kwani alitoweka kwao tangu mwaka 1996 na kuelekea nchini Uganda na mumewe.

Agnes Nelima, mwenye gauni la Kitenge akiwa na ndugu zake

Nelima alibaini kwamba wazazi wake na baadhi ya ndugu zake waliaga dunia kufuatia uzee na wengine waliangamizwa na magonjwa, huku Mzee wa Mtaa huo Richard Wafula, akisema kuwa licha ya kurejea nyumbani baada ya miaka mingi, hatofanyiwa tambiko lolote kwani matambiko hufanyiwa wanaume pekee.

Baadhi ya ndugu waliomuona Agnes, walishangaa kwakuwa walipoteza matumaini ya kumuona tena kwani walihisi alikwishapoteza maisha, baada ya kumsaka kwa muda mrefu bila mafanikio.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents