Burudani ya Michezo Live

Uganda: Mfahamu Mama aliyezaa watoto 44 akiwa na mume mmoja, aandika majina yao kwenye kitabu ili wasiwasahau (Video)

Huko nchini Uganda kuna mama mmoja ambaye amezaa watoto 44 akiwa na mume mmoja ambapo mwanaume huyo baadaye alikiimbia familia hiyo na kumuacha mama huyo akiendelea kuitunza familia.

Mama huyo  akiwa na umri wa miaka 38 mwaka 2018, alikuwa ana watoto 44 kati ya hao watoto 39 walikuwa hai. Wasichana walikuwa kumi na tano na wavulana ni ishirini na tatu.

Mtoto wake wa kwanza alimpata mwaka 1994 na mpaka kufikia mwaka 2018 tayari alikuwa ana watoto 44 .  Alijaribu kutumia uzazi wa mpango lakini dawa hizo zilikuwa zinamkataa na ndipo alipoamua kuzaa.

Kwa sasa Mama Mariam Nabatanzi watoto hao wanawalea peke yake kwani baba watoto wake alimkimbia.

Hata hivyo alidai kuna wanaume wengi walikuwa wanatoka awazalie watoto lakini yeye hakutaka kufanya jambo hilo.

Source: Citizen TV

 

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW