Lifestyle

UGANDA: Mzee wa miaka 94, mwenye watoto zaidi ya 100 na wake 19 aongeza wake wanne

UGANDA: Mzee wa miaka 94, mwenye watoto zaidi ya 100 na wake 19 aongeza wake wanne

Mzee Nulu Ssemakula kijiji kiitwacho Ruyonza nchini Uganda amewashangaza watu kwa kuongeza si mke mmoja wala wawili bali wake wanne.

Hatua ya mzee huyo mwenye miaka 94 imekuwa ya kipekee katika kijiji hicho ambacho jamii yake imekuwa na ndoa ya mke zaidi ya mmoja,naye alikua akizingatia sana masuala ya familia na dini.

Alikuwa muislamu wa kwanza kutoka kujiji cha Ruyonza kwenda kuhiji Maka mwaka 1977, Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeeleza.

Ssemakula anajivunia kuwa kuwa na wake 19 ambao amepata nao zaidi ya watoto 100, mdogo kabisa akiwa na umri wa miezi kumi na mke mdogo kabisa akiwa na miaka 24, ambaye ni mja mzito.

Hivi sasa anaishi na watoto wake wadogo 66.

Wakati baadhi ya watoto wake wana wajukuu, na mzee huyu anasema bado ana matumaini ya kuwa na watoto zaidi na hata wake wengi zaidi.

Mzee Ssemakula alioa mke wa kwanza mwaka 1952, ambaye baada ya muda mfupi tu akaoa wengine watano. Bado wanaishi pamoja. Daily Monitor limeeleza.

HarusiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

”Kwa bahati mbaya niliwapoteza wake zangu wanne ambao walinihitaji zaidi ya uwezo niliokuwa nao, nikawaacha waende. Lakini waliniacha na watoto. Bado nitaoa tena ikiwa nitaishi miaka mingi zaidi na hata kuwa na watoto wengi zaidi.Ninafurahishwa sana na watoto na wake, ndio utajiri wangu wa kweli,” anasema .

Mzee huyu amejenga msikiti na shule, Shule ya msingi Kiyombero, mashine ya kubangua kahawa na mashine ya kupoza maziwa katika kijiji ili aweze kuhudumia familia yake.Akiwa amezungukwa na makazi ya watoto na wajukuu zake, nyumba yake ni kubwa zaidi ikiwa imeezekwa kwa mabati.

Ssemakula huongea huku akiwa na nguvu mithili ya kijana, mcheshi sana kwa wageni, watoto wake na wake zake hucheka sana wanapokuwa wanasikiliza vichekesho vyake ingawa huvisikia mara kwa mara.

”Unapokuwa na wake wengi na watoto wengi, ni kama kuendesha nchi, unapaswa kuomba hekima kuiendesha” anasema Ssemakula.

Changamoto kubwa ambayo ameshawahi kukutana nayo mzee huyu si kuwa na familia kubwa, bali kupoteza mifugo yake katika vita vya waasi mwaka 1979.

Pamoja na kuwa familia kuwa kubwa amemudu kuwasomesha watoto wake, familia yake ina wahandisi, madaktari, wauguzi, maafisa afya, waalimu na wanasheria, wengine wamepitia vyuo vyaufundi huku wengine wakiwa wafanya biashara.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents