Burudani

Uganda yang’ara kwenye shindano la East Africa’s Got Talent msimu wa kwanza, Rais Museveni atuma pongezi kwa washindi

Kundi la watoto wawili la Esther & Ezekiel kutoka Uganda kwa mara ya kwanza limefanikiwa kushinda shindano la East Africa’s Got Talent 2019.

Kwenye fainali hiyo, Uganda ilifanikiwa kuingiza makundi matatu ambayo ni DNA, Singers Jehovah Shalom Acapella na washindi Esther & Ezekiel.

Washiriki wengine waliofika fainali ni Intayoberana kutoka Rwanda, Jannell Tamara na kundi la Spellcast kutoka Kenya.

Mshindi wa msimu huu wa kwanza wa shindano hilo, Esther & Ezekiel wameibuka na kitita cha dola $50,000 ambazo ni sawa na Tsh. Milioni 115 .

Kufuatia ushindi huo, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewapongeza washindi hao kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika “Wajukuu zangu wameniambia kuhusu vipaji vya Esther & Ezekiel, Ambao jioni ya leo wameshinda shindano la East Africa’s Got Talent, Nawapongeza sana,”.

Majaji wa msimu wa kwanza walikuwa ni Vanessa Mdee kutoka Tanzania, Jeff Koinange kutoka Kenya, Gaetano Kagwe (Uganda) na Contact Makeda (Rwanda).

https://www.instagram.com/p/B3TxkoOBD_q/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents