Fahamu

Ugonjwa mpya waibuka China, watokea kwa Nguruwe

Ugonjwa mpya waibuka China, watokea kwa Nguruwe

Ugonjwa mpya wa mafua ambao unauwezekano wa kuwa janga umetambuliwa nchini China na wanasayansi.

Mlipuko huo umejitokeza hivi karibuni na upo miongoni mwa nguruwe lakini hata binadamu wanaweza kuambukizwa, wameeleza wanasayansi.

Watafiti wana wasiwasi kuwa hali inaweza kubadilika na kuweza kusambaa kiurahisi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine na kusababisha mlipuko wa ugonjwa duniani.

Wanasema tatizo hili si kwamba litatokea kwa haraka, lakini kuna uwezekano mkubwa wa maambukizi kuambukiza binadamu na hivyo kuna uhitaji wa ufuatiliaji wa karibu.

Kwa sababu ni ugonjwa mpya, watu watakuwa hawana kinga ya virusi hivyo au iko kidogo.

Wanasayansi wameandika katika jarila la ‘Proceedings of the National Academy of Sciences’ kuwa hatua za kukabiliana na virusi hivi vya nguruwe ni kufuatilia kwa karibu wafanyakazi wanaofanya kazi katika viwanda vya nguruwe na utekelezaji ufanyike kwa haraka.

Tisho la mlipuko

Aina mpya mbaya ya mafua ni miongoni mwa magonjwa hatari sana ambayo wataalamu wanayafuatilia, hata dunia inapambana kuutokomeza mlipuko uliopo sasa wa virusi vya corona.

Janga la mwisho la mlipuko wa mafua ya ngurue, dunia kukabiliana nalo ni mwaka 2009, ambapo mafua hayo ya nguruwe yalianzia Mexico – kulikuwa hakuna vifo vingi kama wasiwasi uliokuepo kwa sababu watu wengi walikuwa na kinga ya kukabiliana na ugonjwa huo na labda kwa sababu mafua hayo yalikuwa yanafanana na virusi vya mafua mengine ambavyo viliibuka miaka ya nyuma.

Virusi hivyo ambavyo viliitwa A/H1N1pdm09, kwa sasa kuna chanjo ya mwaka mzima ambayo inawapa uhakiki watu kuwa na ulinzi kamili.

Virusi vipya vya mafua vimebainika nchini China vinafanana na virusi vya mafua ya nguruwe vilivyoibuka mwaka 2009 lakini vikiwa na mabadiliko kidogo.

Virusi vinatafutwa kwa sasa huko vya popo wa Thai – wanasayansi wakichukua sampuli ya wanyama hao ili kupata chanzo cha virusi vya corona.

Mpaka sasa, hakuna tishio kubwa lakini Profesa Kin-Chow Chang na wenzie ambao wamekuwa wanafanya utaffiti huo , wanasema ni kitu ambacho inabidi kukifuatilia kwa ukaribu.

Virusi ambavyo watafiti wanaviita G4 EA H1N1, vinaweza kukua na kuambukiza wanadamu kwa mfumo wa hewa.

Wamepata ushahidi wa maambukizi ya hivi karibuni ambapo maambukizi yalianzia kwa watu wanaofanya kazi katika viwanda vya nguruwe nchini wa China.

Kinga ya mafua iliyopo sasa haionekani kutulinda ingawa inaweza kufanya hivyo ikihitajika .

Prof Kin-Chow Chang, anayefanya kazi katika chuo kikuu cha Nottingham nchini Uingereza, ameiambia BBC: “Kwa sasa tunapambana na virusi vya corona , lakini inabidi tuwe makini maana kuna tishio la virusi vipya..”

Ingawa virusi hivi vipya si tatizo ambalo litaanza kwa haraka , alisema: “Tusilipuuzie.”

Prof James Wood, mkuu wa idara ya tiba ya wanyama chuo kikuu cha Cambridge, alisema ni kazi “tatizo limekuja kama kutukumbusha ” kuwa tuko katika hatari ya kupata maambukizi kutoka kwa wanyama

SOURCE BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents