Michezo

Uhakika wa Unai Emery kusalia Arsenal kujulikana mwisho wa msimu, David Beckham ammendea Kylian Mbappe

Kazi ya kocha, Unai Emery ndani ya Arsenal huenda ikawa hatarani iwapo kikosi chake kitashindwa kufuzu katika michuano ya UEFA Champions League na ili kuweza kushiriki ni lazima kumaliza katika nafasi nne za juu mwekenye msimamo wa ligi kuu Uingereza ambapo ndipo atakuwa amejikatia tiketi. (Times – subscription required)

Image result for unai emery

Kwa sasa Arsenal ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 15, wakati vinara wa ligi Liverpool wakiwa na alama 24, Man City ikishika nafasi ya pili kwa pointi 16.

Nyota wa zamani wa Manchester United na aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, David Beckham anammendea mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kuwa mteja wake wa kwanza katika kazi yake mpya uwakala wa wachezaji. (Mail)

Image result for David Beckham tobe Kylian Mbappe agent

Miamba ya soka nchini Hispania, Real Madrid imehusishwa kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Denmark, Christian Eriksen dirisha lijalo la usjili la mwezi Januari.(Marca)

Klabu hiyo pia wanaisaka saini ya mshambuliaji kinda wa Red Bull Salzburg mwenye umri wa miaka 19, raia wa Norway, Erling Haaland ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester United. (AS)

Beki wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast, Serge Aurier 26, amesema kwamba alitaka kuondoka mjini London mwishoni mwa msimu uliopita na kukiri kuwa mpaka sasa hajui hatma yake iko vipi katika klabu hiyo. (Football.London)

Aston Villa imehusishwa na kutaka kusaini ya kiungo wa kati wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza Eric Dier, 25. (Birmingham Mail)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents