Michezo

Uholanzi yailaza Brazil 3-0,Uholanzi yashika nafasi ya 3 kombe la dunia

Timu ya taifa ya Uholanzi imeibamiza Brazil 3-0 na kutwaa nafasi ya tatu katika kombe la dunia huko Brazil.
140712221327_medalhas_holanda_512x288_getty
Mashabiki wa Brazil waliwazomea wachezaji wao akiwemo kocha Luiz felipe Scolari kwa utendakazi duni katika mechi hizi mbili za mwisho ambazo Brazil imefungwa mabao 10 nayo ikifunga moja.

Brazil ilifungua mechi hiyo kwa kasi lakini ikafungwa bao la kwanza kunako dakika ya pili kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na Robin va Persie.

Nahodha Thiago Silva alimtega Arjen Robben nje ya eneo lakini refarii kutoka Algerian Djamel Haimoudi akaamua kumwadhibu kwa kadi ya njano na penalti dakika mbili tu baada ya mechi hiyo kuanza badala ya kumwonesha kadi nyekundu .

Mashambulizi ya Uholanzi yalizaa matunda kunako dakika ya 15 ya mechi hiyo David Luiz alipookoa mkwaju uliokuwa unaelekea wavuni kwa kichwa lakini ukamwangukia Daley Blind naye akaurejesha wavuni.

Kila mtu uwanjani alifurahia Brazil walipofanya mashambulizi kwenye lango la Uholanzi lakini kila mara walipofika katika eneo walikosa makali na kushindwa kupenyeza safu ya ulinzi ya Uholanzi.

Hata hivyo Georginio Wijnaldum aliifungia Uholanzi bao la tatu na kumpa kocha Louis va Gaal kwaheri na nishani ya shaba kutoka kwa fifa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents