Uncategorized

Uhuru Selemani akamilisha usajili kwenye klabu hii Afrika Kusini

Mshambuliaji wa Tanzania, Uhuru Selemani Mwambungu amejiunga na klabu ya Royal Eagles FC ya Afrika kusini kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mchezaji huyo amejiunga na timu hiyo kama mchezaji huru baada ya kuachana na klabu ya Biashara United ya Mara.

Kabla ya kurejea Tanzania Uhuru alikuwa anacheza Royal Eagles na January 2018 alijiunga na African Lyon iliyokuwa ligi daraja la kwanza (FDL) na August 2018 akajiunga na Biashara United ya Mara -Kila la Kheri Uhuru.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mchezaji huyo wa Kimataifa wa Tanzani ameishukuru klabu yake ya zamani ya

”KWANZA KABISA NIMSHUKURU MOLA MLEZI KWA HATUA HII TENA …. pili niwashukuru mashabiki wangu ambao mmekuwa hampendi kuniona nikirudi chini ahsanteni sana … lkn pia shukran za kipekee ziwaendee mashabiki wa @biasharaunited09 na wachezaji kwa kuishi na mm kw aupendo ktk kipindi kifupi mwenyezi mungu awasimamie ktk kila jambo lenu,” ameandika Uhuru Selemani kupitia akaunti yake ya Instagram.

Uhuru ameongeza ” lkn shukran za dhati kabisa zimwendee mkurugenzi na mmiliki wa timu ya @african_lyon_footbal_club
@zamundakangezi  kwa kuweza kuniruhusu bila kipingamizi ilhali tumedumu kwa muda wa week mbili tu Ahsante sana… @royaleaglesfc im proud to be part of the family again thank you so much .”

Royal Eagles FC inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza (FDL) nchini Afrika Kusini.



https://www.instagram.com/p/BsYbARRgKwB/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents