Burudani ya Michezo Live

UINGEREZA: Afisa wa polisi ashitakiwa kwa kumuua mchezaji wa mpira wa miguu – Video

UINGEREZA: Afisa wa polisi ashitakiwa kwa kumuua mchezaji wa mpira wa miguu - Video

Afisa wa polisi ameshtakiwa wa mauaji ya mchezaji soka wa zamani Dalian Atkinson ambaye alikufa baada ya kupigwa shoti ya umeme.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 48, alikamatwa katika nyumba ya baba yake katika eneo la Telford, Shropshire, tarehe 15 Agosti 2016.

Afisa wa pili wa polisi pia kutoka West Mercia , ameshtakiwa kwa mateso yaliyosababisha madhara kwa mwili.

Polisi hao kwa pamoja wamefikishwa katika hakimu wa mahakama ya Birmingham.

Dalian AtkinsonDalian Atkinson alianza kucheza mpira katika timu ya Ipswich katika miaka ya 1980

Waendesha mashtka walifanya uamuzi kufuatia upelelezi ulioafanywa na kitengo cha polisi kinachofuatilia mienendo ya poli nchini Uingereza (IOPC).

Polisi haikuwataja majina maafisa hao wawili kwasababu inafahamika kuwa kujitetea kwao kutabakia kuwa siri.

Mmoja wa maafisa hao ameshtakiwa kwa mauaji na waendehsamashtaka ambaye wamempatia jina bandia ”Afisa A” .

Alikana mashtaka dhidi yake baada ya kufika mbele ya hakimu na kurejeshwa mahabusu.

Afisa wa pili , ‘Afisa B’, pia ameashiria kuwa atayakana mashtaka dhidi yake na alipewa dhamana kabla ya kurejea tena baadae katika mahakama ya Birmingham.

Familia ya Atkinson ilijulishwa , msemaji wake akasema na akatoa taarifa ya kuafiki uamuzi lakini “wanasikitika kwamba tayari zaidi ya miaka mitatu imepita tangu kilipotokea kifo Dalian “.

Fans tributeMahsabiki wa Aston Villa walitoa heshma zao za mwisho kwa mshambuliaji wa zamani

Maafisa wa polisi walikua eneo la Meadows Close katika eneo la Telford, ambako Bwana Atkinson alikamatwa nje ya kwao majira ya saa saba unusu usiku.

Alipelekwa kwa gari la wagonjwa hadi katika hospitali ya Princess Royal ambako afariki baadae.

Ndugu zake walisema kuwa mchezaji soka huyo alikuwa ana matatizo mbali mbali ya kiafya na alikuwa na moyo dhaifu wakati alipopigwa na nguvu za umeme.

Bwana Atkinson alianzia taaluma yake ya soka katika timu ya Ipswich Town kabla ya kuhamia Sheffield Wednesday, Real Sociedad, Aston Villa na Fenerbahçe nchini Uturuki

Anakumbukwa sana kwa kufunga goli katika mechi ya sikuya msimu 1992-93 wakati alipoupepeta mpira kutoka katikatiya uwanja kabla ya kuumchenga golikipa wa Wimbledon katika eneo la penati na kuutingisha wavu.

goli lake la kihistoria

Katika taafifa yake Mkuu wa polisi wa West Mercia alisema kuwa : “Mawazo yetu yanaendelea kubakia na familia na marafiki wa Dalian Atkinson katika kipindi hiki kigumu”.

Mkuu wa polisi Anthony Bangham amesema kuwa haitakuwa vema kutoa kauli kuhusiana na kifo cha Bwana Atkinson, lakini akaongeza kuwa atahakikisha maafisa husika “Wanausaidizi unaofaa katika kipindi chote cha mchakato wa kisheria unaohusiana na uhalifu “.

Histori ya Dalian Atkinson katika soka

Dalian AtkinsonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
  • Dalian Atkinson alianzia kucheza mpira katika Ipswich
  • Alisaini mkataba na Sheffield Wednesday wa pauni £450,000 mnamo mwaka 1989
  • Kwa mara ya kwanza alicheza soka la kimataifa katika mchezo baina ya timu B ya England mwaka 1990, dhidi ya Ireland
  • Agosti 1990 Atkinson alihamia Uhispania , alipojiunga na Real Sociedad kwa malipo ya pauni milioni £1.7
  • Ron Atkinson alisaini mkataba kwa mara ya pili Julai 991 – uliomrejesha tena England kuchezea Aston Villa
  • His strike against Wimbledon was named the goal of the 1992-93 season
  • Atkinsonalijiunga na ligi ya Uturuki akichezea timu ya Fenerbahçe mnamo mwaka 1995, lakini alishindwa kukaa huko
  • HAliichezea Manchester City pamoja na klabu za Saudi Arabia na Korea Kusini

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW