Michezo

Uingereza kushuka dimbani Jumapili hii bila Joe Hart

Mlinda lango wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Stoke City, Jack Butland anatarajiwa kuanza katika mchezo wa mwisho dhidi ya Lithuania utakaochezwa hapo kesho siku ya Jiumapili kuwania tiketi ya kucheza michuano ya kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2108.

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amempendekeza golikipa huyo mwenye umri wa miaka 24 kuchukua nafasi ya Joe Hart.

Southgate amesema kuwa kijana huyo yupo vizuri na anamorali kubwa na anadhani hiyo ni nafasi muhimu kwake kufanya vizuri zaidi.

Uingereza ilichomoza na ushindi wa 1-0 mbele ya Slovenia katika mchezo wake wa mwisho kwa bao lililofungwa na nahodha wao, Harry Kane dakika za majeruhi na kuifanya kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urisi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents