Michezo

Uingereza na Venezuela uso kwa uso fainali ya kombe la dunia U-20

Timu ya taifa ya Uingereza imetinga katika hatua ya fainali ya kombe la dunia kwa vijana walio na umri chini ya miaka 20 (U-20) baada ya kuifunga Italia kwa mabao 3-1.

Katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jeonju huko Korea Kusini, Uingereza ilifanikiwa kufunga magoli yake kupitia kwa Dominic Solanke aliyefunga mara mbili na Ademola Lookman huku goli la kufutia machozi la Italia likifungwa na Riccardo Orsolini.

Wakati huo huo, timu ya taifa ya Venezuela na wao wametinga katika hatua hiyo ya fainali baada ya kuiitoa Uruguay kwa jumla ya penati 4-3 baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1-1 katika dakika 120.

Mchezo wa fainali kati ya Uingereza na Venezuela utachezwa Jumapili hii ya Juni 11 katika uwanja wa Suwon ambapo kabla ya mchezo huo utatanguliwa na mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu kati ya Uruguay na Italia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents