Technology

Uingereza: Televisheni ya zamani (Analog) yaelezwa kuvuruga mtandao kwa zaidi ya miezi 8 (+Video)

Kitendawili cha kijiji kimoja kupoteza mawasiliano ya intaneti kila saa moja asubuhi kiliteguliwa baada ya wahandisi kugundua tatizo lilikuwa likisababishwa na televisheni ya zamani.

Mkazi wa Aberhosan ambaye jina lake halikutajwa, amesema hakuwa na habari televisheni yake ya zamani ilikuwa inavuruga mawasiliano katika kijiji kizima.

Baada ya miezi 18 wahandisi walianza kuchunguza kwa kina tatizo hilo baada ya mpango wa kuweka upya nyaya za mawasiliano kufeli.

Mwenye televisheni hiyo aliahidi kuacha kuitumia.Kijiji hicho sasa kina huduma imara ya intaneti.

Wahadisi wa shirika la Openreach walikuna vichwa kuelewa kwa nini tatizo hilo lilikuwa linaendelea kujitokeza hadi pale walipotumia kifaa maalum kilichowasidia kung’amua hitilafu ilikuwa wapi.

Mkazi huyo ambaye alikuwa akitumia televisheni ya zamani ambayo alikuwa akiiwasha kila siku saa moja asubuhi – bila ya kuwa na ufahamu televisheni hiyo kuu kuu ilikuwa inaathiri mawasiliano.

Mmiliki wa televisheni hiyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe “alishangaa” sana kujua ni televisheni yao ya zamani iliokuwa inasababisha tatizo hilo, kwa mujibu wa Openreach.

“Walikubali kuizima na kuahidi kwamba hawataitumia tena,” alisema mhandisi Michael Jones.

Wahandisi walizunguka kijiji hicho kwa kutumia kifaa maalum kutafuta chanzo cha “hitilafu” hiyo na kurekebisha.

“Ikifika saa moja asubuhi, tunasikia mlio fulani,” alisema bwana Jones.

“Kifaa chetu kiling’amua tatizo kubwa ambalo lilikuwa likiathiri umeme katika kijiji hicho.

“Ilibainika kuwa kila asubuhi mwendo wa saa moja mkazi huyo alikuwa anawasha TV yake ya zamani, ambayo ilikuwa inapoteza mawasiliano ya intaneti katika kijiji kizima.”

Televisheni hiyo ilipatikana inatoa mlio fulani wa kiwango cha juu (SHINE), ambao unahitilafiana na nguvu za umeme kufikia vifaa vingine.

Bwana Jones amesema tatizo hilo halijashuhudiwa tena tangu chanzo chake kilipogunduliwa.

Nini kingine kinaweza kuleta tatizo la mawasiliano?

Bwana Jones amesema tatizo hilo halijashuhudiwa tena tangu chanzo chake kilipogunduliwa
Bwana Jones amesema tatizo hilo halijashuhudiwa tena tangu chanzo chake kilipogunduliwa

Suzanne Rutherford, Mhandisi mkuu wa Openreach huko Wales, alisema kitu chochote kinachotumia umeme – kuanzia taa ya ndani ya microwave – inaweza kuathiri mawasiliano.

“Tunatoa ushauri kwa umma kuhakikisha vifaa vya kielektroniki wanavyotumia vimeidhinishwa na vinafikia viwango vya sasa vya ubora nchini Uingereza,” alisema.

“Na ikiwa vina hitilafu, wasilisha ripoti kwa watoa huduma ili wachukue hatua.”

https://www.instagram.com/tv/CFrFSVfhALy/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents