Habari

Uingereza yachukuliwa hatua za kiseheria na Umoja wa Ulaya

Umoja wa Ulaya leo umechukua hatua za kisheria dhidi ya Uingereza kufuatia mipango ya nchi hiyo ya kutunga sheria itakayokiuka sehemu ya mkataba wa Brexit uliotiwa saini mwaka uliopita.

An EU supporter waves a flag in front of parliament in London, September 30, 2020. The ninth round of trade talks between the EU and Britain have started in Brussels as the two sides continue to clash over the controversial UK internal market bill [Frank Augstein/AP]

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema mpango huo wa Uingereza ni ukiukaji wa wazi wa nia njema iliyoahidiwa na kila upande katika makubaliano ya nchi hiyo kujitoa kutoka Umoja Umoja, Brexit.

Von der Leyen amesema iwapo muswada huo tata kuhusu soko la ndani la Uingereza utaidhinishwa utazusha mparaginyiko kwenye itafiki kuhusu Ireland mbili iliyoafikiwa katika mkataba wa Brexit.

Umoja wa Ulaya una wasiwasi kuwa sheria hiyo inaweza kurejesha vikwazo vya kibiashara na uhamiaji kwenye mpaka kati ya Ireland Kaskazini iliyo sehemu ya Uingereza na Jamhuri ya Ireland iliyo mwanancha wa kanda ya Ulaya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents