Uncategorized

Uingereza yapewa miezi sita kujitoa umoja wa Ulaya

Viongozi wa Ulaya wamekubaliana na Uingereza kuchelewesha muda wa Brexit kwa miezi sita, na kuliepusha bara hilo na kile kingekuwa ni kuondoka Uingereza kwa njia ya vurugu bila ya makubaliano mwishoni mwa wiki hii.

Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk amethibitisha kuwa Uingereza mara hii imepewa hadi Oktoba 31 kukamilisha mchakato wa kuondoka rasmi.

Makubaliano hayo yaliyofikiwa usiku wa kuamkia leo mjini Brussels, yana maana kuwa kama Uingereza itabaki katika Umoja wa Ulaya baada ya Mei 22, itahitajika kushiriki katika uchaguzi wa Ulaya – au iondoke bila ya makubaliano mnamo Juni mosi.

Waziri Mkuu Theresa May amesema ataendelea kufanya kazi ili mpango wake wa kujiondoa uidhinishwe na bunge na kuhakikisha kuwa makubaliano hayo yanakamilika kwa njia nzuri.

Atalihutubia bunge leo kabla ya maafisa wake kukutana kwa ajili ya mazungumzo zaidi na chama cha upinzani cha Labour, ili kujaribu kupata ufumbuzi wa mkwamo huo wa kisiasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents