Michezo

Uingereza yashindwa kutamba michuano ya Luxembourg Open

Wachezaji tenis raia wa Uingereza, Heather Watson na Naomi Brady kwa pamoja wametupwa nje ya michuano ya wazi ya Luxembourg (Luxembourg Open ) hatua ya robo fainali.

Mchezaji tenis raia wa Uingereza, Heather Watson

Watson ambaye anashika nafasi ya pili katika viwango vya ubora wa mchezo huo nchini Uingereza amekubali kipigo hicho kwa jumla ya seti 6-4 6-4 dhidi ya mwana dada Elise Mertens raia wa belgiji.

Wakati kwa upande wa muingereza mwenzake, Naomi Broady amekubali kipigo cha jumla ya seti 6-0 5-7 6-1 kutoka Monica Puig raia wa Puerto Rico.

Sasa wawili hao waliyoshinda mchezo huo war obo fainali, Puig na Elise Mertens watakutana katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya wazi ya Luxembourg (Luxembourg Open ).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents