Habari

Uingereza yaipa Iran onyo hili kali baada ya kushikilia meli yao ya mafuta

Uingereza yaipa Iran onyo hili kali baada ya kushikilia meli yao ya mafuta

Iran huenda inachagua “njia hatari ” ya mwenendo wa ” kukiuka sheria na kuvuruga mambo ” baada ya maafisa wake kuiteka meli yenye bendera ya Uingereza kwenye eneo la Ghuba, amesema waziri wa mambo ya nje wa uingereza. Wamiliki wa meli hiyo inayofahamika kama Stena Impero wameshindwa kuwasiliana meli hiyo ambayo ilikuwa imezungukwa na eneo muhimu la Strait of Hormuz.

Kwamujibu wa BBC. Serikali ya Uingereza imesema kuwa “inahofu kubwa” juu ya hatua ”zisizokubalika” za Iran.

Iran imesema kuwa chombo hicho kilikuwa “kinakiuka sheria za kimataifa za vyombo vya majini”.

Stena ImperoHaki miliki ya pichaERWIN WILLEMSE
Image captionStena Impero, meli ya yenye bendera ya Uingereza iliyotekwa na Iran kwenye eneo la Ghuba

Meli ya pili ya mafuta ya Uingereza iliyokuwa na bendera ya nchi ya Liberia ,MV Mesdar, pia ilivamiwa na walinzi waliokuwa na silaha lakini baadae Ijumaa iliachiliwa.

Ni nini kilichotokea ?

Stena Impero ilikamatwa na wanajeshi wa Iran al maarufu Iranian Revolutionary Guard siku ya Ijumaa katika eneo muhimu la maji katika Ghuba.

Meli hiyo ya mafuta ilizingirwa na meli nne na helikopta kabla ya kuelekezwa katika eneo la maji la Iran, amesema Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt.

Amesema kuwa “uhusu wa kusafiri majina lazima uimarishwe” na akaonya kuwa itakuwa na ” athari mbaya ” kama hali haitatatuliwa haraka..

” Hatuangalii hatua za kijeshi ,” na kuongeza kuwa: “Tunatafuta njia za kidiplomasia za kutatua hali hii.”

Meli ya MesdarHaki miliki ya pichaNORBULK SHIPPING
Image captionMeli ya Mesdar

Jumamosi Bwana Hunt alituma ujume wa twitter uliosema: ” hatua ya jana katika eneo la Ghuba inaonyesha ishara za wasi wasi , Iran inaweza kuwa inmechukua mkondo hatari wa kuyumbisha hali kinyume cha sheria baada ya kumamatwa kwa meli ya mafuta katika eneo la Gibraltar kuelekea Syria.”

Shirika la habari linalomilikiwa na taifa la Iran IRNA limesema kuwa meli hiyo ya mafuta ilikamatwa baada ya kugongana na boti la uvuvi na kushindwa kujibu mawasiliano ya meli nyingine ndogo.

Mmiliki wa meli hiyo alisema kuwa ilikuwa inatekeleza kikamilifu masharti na sheria na ilikuwa katika eneo la maji la kimataifa ilipovamiwa na kutekwa.

Imesema kuwa hakuna taarifa za majeruhi miongoni mwa wahudumu wa meli hiyo 23, ambao walikuwa uraia wa mataifa ya India, Urusi, Latvian na Ufilipino.

Msemaji wa serikali ya Uingereza ameiambia BBC kuwa : “tumeshauri meli za mizigo za Uingereza kuwa mbali na eneo la Ghuba kwa muda .”Chombo cha kampuni ya Stena Impero ilikuwa ikisafiri majini ikiwa na bendera ya Uingereza na kusajiliwa London.

”Balozi wetu mjini Tehran anfanya mawasiliano na wizara ya mambo ya kigeni wa Iran kutatua hali hii na tunafanya kazi kwa karibu na washirika wetu wa kimataifa,” alisema.

Ni nini chanzo cha yote haya? :

Stena ImpereroHaki miliki ya pichaSTENA BULK
Image captionStena Imperero

Tukio hili limefanyika wakati kukiwa na mvutano kati ya Uingereza, Marekani na Iran.

Jeshi limesema meli hiyo imekamatwa kwa kuvunjwa kwa sheria tatu: kuzima GPS; kuingia kwenye mpaka kupitia njia ya kutokea badala ya kuingilia; na kupuuzia maonyo.

Taarifa zinasema hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi na usalama wa wafanyakazi ni jambo la kwanza kwa wamiliki na mameneja.

Tarehe 9 mwezi Julai, Uingereza ilieleza tishio la usalama katika maji ya Iran kwenye Ghuba ni ”kubwa”.

Wakati huohuo, Marekani imedai kuwa imedungua ndege isiyo na rubani kwenye Ghuba, baada ya Iran kushambulia ndege isiyo na rubani katika eneo hilo mwezi Juni.Raisi wa Marekani Donald Trump amesema atazungumza na Uingereza kufuatia madai kuwa Iran imeikamata meli iliyosajiliwa nchini Uingereza.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents