Habari

Ujenzi wa nyumba za Magomeni kota waanza kutekelezwa

Ahadi ya Rais John Magufuli ya kujenga nyumba 644 katika eneo la Magomeni Kota, jijini Dar es Salaam, ndani ya mwaka mmoja imeanza kutekelezwa.

wadaiwa-1

Wakala wa majengo Tanzania (TBA) , Elius Mwakalinga,ametoa ufafanuzi jijini Dar es salaam jinsi walivyopokea maelekezo hayo kutoka kwa rais Magufuli na kuanza ujenzi wa nyumba hizo usiku na mchana.

“Mheshimiwa rais alituelekeza wakala wa majengo tujenge kwa ajili ya kuwapatia majengo wakazi wa Magomeni Kota ambao walibomolewa maeneo yao sasa kutokana na maagizo, maana yake ametupatia juzi kuamkia jana, tulilazimika kuja hapa na kufanya kazi usiku na mchana, na sasa hivi nimepita hapa kujihakikishia kwa wale wasaidizi wangu kama kweli wanaendelea usiku huu kufanya kazi kwasababu unaweza ukalala kumbe watu nao wamelala,”alisema Mwakalinga.

Takribani wiki tatu zimepita, tangu Rais Magufuli atoe ahadi hiyo. Baada ya miezi miwili mradi wa nyumba 644 kwenye eneo la Magomeni kota utaanza kujengwa na wakazi walioathirika kuishi bure kwa muda wa miaka 5.

Ujenzi huo utagharimu shilingi bilioni 20.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents