Ujerumani kujenga bomba ‘refu’ la kusafirisha bia
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni!! Wakati nchi yetu ya Tanzania ikiingia mkataba na Uganda kwa ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta kutoka mjini Hoima hadi Tanga hii tofauti kabisa na ujerumani ambapo hao wapo mbioni kujenga bomba la kusafirishia pombe kama hujui basi acha nikung’ate sikio.
Waandaaji wa Tamasha moja maarufu la muziki wa rock lijulikanalo kama Wacken Open Air Festival nchini Ujerumani wamewahakikishia wateja wao laki moja (100,000) kwamba, kamwe msimu huu mpya hawatokumbwa na uhaba wa pombe kwani watajenga bomba refu la kusafirisha kinywaji hicho maeneo yote kutakakofanyika tamasha hilo.
Taarifa kutoka mtandao wa Metal Insider zinasema mbomba hilo litakuwa na urefu wa Kilometa 7 na upana wa nchi 14, huku likitarajiwa kutoa lita 6 za pombe kwa sekunde moja.
Maamuzi ya kujenga bomba hilo la pombe yamekuja baada ya malalamiko kutoka kwa wahudhuriaji wa tamasha hilo wakidai kila mwaka limekuwa likishindwa kuwahudumia vinywaji vya kutosha kitu ambacho kinasababisha bei ya vinywaji kuongezeka maradufu.
Ujenzi wa bomba hilo utagharimu kiasi cha Euro milioni 1 sawa na shilingi bilioni 2.5 za kitanzania huku likitarajiwa kukamilika mwezi July siku chache kabla ya Tamasha hilo kuanza.
Ujerumani inakadiliwa kuwa ni nchi ya 3 kwa utumiaji wa pombe duniani ambapo kila mwaka mwananchi mmoja hutumia lita 115.5 za pombe ikiwa nyuma ya nchi za Ireland na Jamhuri ya Czech.
Tamasha la Wacken Open Air festival ni moja ya matasha makubwa ya muziki wa Rock duniani ambapo mwaka huu litafanyika Tarehe 3-5 ya mwezi Augosti kwenye viunga vya mji wa Schleswig-Holstein kaskazini mwa Ujerumani na baadhi ya wasanii watakaotumbuiza ni wakongwe Marilyn Manson na Status Quo.