Michezo

Ujerumani ‘Out’ kombe la dunia nchini Urusi

Bingwa mtetezi wa michuano ya kombe la dunia timu ya taifa ya Ujerumani imeyaaga mashindano rasmi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2 – 0 kutoka kwa Korea Kusini.

Ujerumani ilihitaji pointi tatu kwenye mchezo wa leo dhidi ya Korea Kusini ili kujihakikishia kuendelea kutetea ubingwa wake lakini ikashindwa kufanya hivyo baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kutoka kwa wachezaji Kim Young-Gwon aliyefunga dakika ya (90+2) na Son Heung – Min akihitimisha karamu hiyo dakika ya (90+6) yote yakipatikana wakati wa nyongeza kabla mpira kumalizika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents