Siasa

Ujerumani yatoboa siri kubwa, kiongozi wa upinzani Urusi alitiliwa sumu ya Novichok

Kuna ushahidi uliodhahiri kuwa mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny alipewa sumu ya Novichok inayoathiri neva, Ujerumani imesema. Chansela Angela Merkel alisema kuwa mwanasiasa huyo alinusurika kuuawa na dunia itatafuta majibu kutoka kwa Urusi.

Bwana Navalny alisafirishwa Ujerumani baada ya kuanza kuugua akiwa ndani ya ndege huko Siberia mwezi uliopita na bado hadi sasa amepoteza fahamu.

Timu yake inasema alitiliwa simu kwa maagizo ya Rais Vladimir Putin. Hata hivyo Urusi imekanusha madai hayo.

Msemaji wa Urusi aliitaka Ujerumani kuishirikisha taarifa zake zote huku msemaji wa wizara ya mambo ya nje Maria Zakharova akilalamika kwamba madai ya Novichok hayakuambatinishwa na ushahidi wowote. “Ukweli uko wapi, ni mchakato gani uliotumika, yaani hata mutoe taarifa?” alisema.

Sumu inayoathiri neva ya Novichok ilitumiwa kwa aliyekuwa jasusi wa Urusi Sergei Skripal na binti yake wakiwa Uingereza mwaka 2018. Ingawa wao walinusurika, mwanamke mwingireza alifariki baadae akiwa hospitalini. Uingereza ilishutumu jeshi la Uingereza kwa kutekeleza shambulio hilo.

Waziri Mkuu Boris Johnson alishutumu shambulio la hivi karibu na kulitaja kama aibu. Serikali ya Urusi sasa ni lazima ielezee nini kilichotokea kwa Bwana Navalny – tutashirikiana na washirika wa kimataifa kuhakikisha haki inatendeka” aliandika kupitia ujumbe wa Twitter.

Ujerumani imesema nini?

Baada ya serikali ya Ujerumani kutoka matokeo ya vipimo vya kubainisha ikiwa mwanasiasa huo alitiwa sumu vilivyofanyika katika maabara ya kijeshi ya Chansela Merkel alisema kwamba “sasa kuna maswali nyeti ambayo ni serikali ya Urusi tu inaweza na ni lazima ijibu”.

“Baadhi walijaribu kumnyamazisha Bwana Navalny na kwa niaba ya serikali yote ya Ujerumani, nashutumu hilo kwa nguvu yote.”

Chansela Merkel alisema washrika wa Ujerumani Nato na EU wamefahamishwa matokeo ya uchunguzi huo na wataamua hatua ya pamoja stahiki ya kuchukua kulingana na jinsi Urusi itakavyojibu.

Mke wa Navalny, Yulia Navalnaya na balozi wa Ujrusi nchini Ujerumani pia watafahamishwa kuhusu matoke ohayo serikali ya Ujerumani imesema.

Muungano wa Ulaya imetaka uchunguzi wa wazi kufanywa na serikali ya Urusi. “Walihusika lazima wawajibishwe,” taarifa hiyo imesema.

Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg pia alitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kupitia ujumbe aliandika kwenye mtandao wa Twitter, huku Baraza la Taifa la Usalama Marekani, likisema tukio hilo linaloshukiwa kuhusisha sumu ni aibu na halikubaliki kabisa”.

“Tutashirikiana na washirika wengine na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha waliotekeleza kitendo hicho huko Urusi wanawajibishwa punde tu ushahidi utakapopatikana na kusitisha ufadhili wa vitendo vyao vya kiovu,” msemaji wa Baraza la Usalama la Marekani amesema.

Kipi kilichomtokea Navalny?

Navalny alikuwa akirejea mjini Moscow akitokea Tosmk.

Wakati akiwa safarini alijihisi mgonjwa. Ndege ililazimika kutua kwa dharura mjini Osmk na kushukiwa kwamba Alexei alipewa sumu.

Wakati huo timu yake ilisema, ”Tunashuku kuwa Alexei ameathirika na kitu ambacho kilichanganywa kwenye chai yake. Ndicho kitu pekee alichokunywa tangu asubuhi.

Navalny akisafirishwa kwenda Ujerumani baada ya kuwepo hospitali ya mjini Omsk nchini Urusi

”Madaktari walisema kuwa sumu hiyo inayeyuka haraka sana kwenye kimiminika cha moto na Alexei akapoteza fahamu.’

Baada ya kutokeakwa tukio hilo, Bwana Navalny aliwekwa kwenye mashine ya msaada wa kupumua huku akiwa hana fahamu.

Ndege iliyokuwa imembeba mkosoaji mkuu wa Putin ililazimika kubadili safari na kuelekea Omsk, ambapo madaktari walimtibu kwa siku tatu pekee kabla ya kuhamishwa hadi hospitali ya Charité mjini Berlin nchini Ujerumani.

Novichok ni nini?

Jina Novichok linamaanisha “mgeni” Kirusi, na ni la sumu kali iliyotengenezwa na e Umoja wa Kisovieti miaka ya 1970 na 1980.

media captionLaura Foster explains how the Novichok nerve agent works

Sumu ya Novichok ina athari saw ana sumu zingine – inafanya kazi kwa kufunga mawasiliano kutoka kwenye neva hadi kwenye misuli na kufanya viungo vingi kushindwa kufanya kazi.

Ikiwa baadhi ya sumu hiyo ni ya majimaji, inaaminika kuna nyingine za vidonge. Hii ikimaanisha kwamba inaweza kutawanywa kama ungaunga.

Sumu ya Novichocks imetengenzwa kuwa na sumu zaidi kuliko silaha za kemikali na hivyo basi baadhi ya sumu hiyo hufanya kazi haraka sana mwilini kati ya sekunde 30 hadi dakika mbili.

Mwaka 2018, Sergei Skripal nab inti yake Yulia walikuwa katika hali mbaya sana katika mji wa Uingereza wa Salisbury, baada ya washukiwa wawili wa Urusi kusemekana kwamba wamewanyunyizia sumu hiyo kwenye kishikio cha mlango katika nyumba ya Bwana Skripal, aliyekuwa jasusi wa Urusi.

Alexei Navalny ni nani?

Alijipatia jina kwa kufichua vitendo vya rushwa akikita chama cha bwana Putin cha United Russia kuwa ”chama cha wezi na wahalifu”, na alitumikia vifungo kadhaa gerezani.

Mwaka 2011 alikamatwa na kufungwa kwa siku 15 baada ya maandamano yaliyodai kuwepo kwa vitendo vya wizi wa kura vilivyodaiwa kufanywa na chama tawala katika kura za ubunge.

Bwana Navalny alitumikia kifungo mwezi Julai mwaka 2013 kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha lakini alisema kuwa hukumu hiyo ilichochewa kisiasa.

Alijaribu kusimama kuwania nafasi ya urais mwaka 2018 lakini alizuiwa kwa kuwa alikuwa tayari amehukumiwa kifungo.

Bwana Navalny alifungwa siku 30 gerezani mwezi Julai mwaka 2019 kwa kosa la kuitisha maandamano ambayo yalikuwa batili.

Nani mwingine aliyewahi kutiliwa sumu?

Kwa mujibu wa BBC. Mwaka 2006, Alexander Litvinenko – aliyekuwa afisa wa kijasusi wa Urusi ambaye aligeuka na kuwa mkosoaji wa Urusi na kukimbilia Uingereza – alifariki dunia baada yachai yake kutiliwa sumu aina ya polonium-210.

Hivi karibuni, wanahabari na mwanaharakati wa upinzani Vladimir Kara-Murza inasemekana kwamba alitiliwa sum umara mbili na vikosi vya usalama Urusi. Nusra afariki dunia baada kupata matatizo ya figo mwaka 2015 na miaka miwili baadae alipoteza fahamu kwa wiki moja.

Mkosoaji mwingine wa Kremlin, Pyotr Verzilov, aliishutumu idara ya ujasusi ya Urusi kwa kumtilia sumu mwaka 2018, alipougua baada ya kusikilizwa kwa kesi, na akapoteza uwezo wake wa kuona na kuzungumza. Yeye pia alitibiwa katika hospitali ya Charité Ujerumani, na aliomba wakfu wa Amani wa Sinema kufanya maandalizi ya kumchukua Bwana Navalny kwa matibabu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents