Ujio mpya wa Q-Chief

Ujio mpya wa Q-Chief
Kichwa cha mwanamziki Q Chief a.k.a Q Chilla sasa ni cheupe kama
kiganja cha mkono kwa kuwa ameamua sasa rasta basi na kuonyoa nywele
zake zote na kubaki na kialaza

Hivi sasa anatamba na kibao chake cha mnanda ambao pia unajulikana kama mchiriku.

Kuonesha upara huo unakwenda sambamba na mabadiliko yake makubwa katika fani ya muziki wa kizazi kipya, amejiunga ndani ya lebo ya studio za Bongo Records ilioko chini ya Prodyuza mahiri kabisa hapa bongo aitwaye P-Funk a.k.a Majani a.k.a Kinywele kimoja.

Sasa hivi bongo Records ina vichwa vipya kabisa, akiwemo Ngwair, Q-Chilla, C-Pwaa na wengine kibao,….kama vile haitoshi wameongeza maprodyuza wengine wakali akiwemo Producer Q na Antonio.

Wadau wa muziki wa bongofleva kaeni mkao wa kula, tutawadondoshea ngoma zao kibao karibuni!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents