MichezoUncategorized

Ujio wa Everton Bongo ni gumzo, Ommy Dimpoz awasubiri kivyake

Ni kweli ujio wa Everton ni habari nyingine kubwa ndani ya soka la Bongo kutokana na ukubwa wa klabu hiyo yenye mafanikio katika ligi kuu ya Uingereza.

Ommy Dimpoz

Klabu hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri ya SportPesa itatua nchini Julai 13 kucheza na timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya ambaye ni mshindi wa mashindano ya SportPesa Super Cup 2017.

Katika mitandao ya kijamii kumekuwa na gumzo mbalimbali kuhusu ujio wa klabu hiyo hasa hasa baada ya jana kiungo machachari wa timu hiyo, Morgan Schneiderlin kupost picha instagram akieleza yupo nchini Tanzania kwaajili ya honeymoon.

Jumanne hii muimbaji wa muziki ambaye anafanya vizuri na wimbo Kajiande, Ommy Dimpoz ameonyesha na yeye ni mmoja kati wa wadau wa michezo wanaousubiria mchezo huo kwa hamu.

“Pale unapopata taarifa kuwa Everton wanakuja. wafollow @tzsportpesa tukaucheki mtanange Liveeeeeeeeee!!!!!!,” alitweet Ommy Dimpoz.

Klabu hiyo ambayo inanolewa na kocha Ronald Koeman, imeshika nafasi ya 7 katika msimu wa 2016/17.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents