Michezo

Ujio wa Everton kuboresha Uwanja wa Taifa (Video)

Kampuni ya michezo ya kubashiri ‘SportPesa‘ imeanza kuthibitisha nia yake ya kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu nchini, baada ya klabu ya mpira wa miguu ya nchini Uingereza Everton, kuthibitisha kutua nchini Julai 13 kwaajili ya mchezo wao dhidi ya bingwa wa michuano ya SportPesa Super Cup.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Everton, Leon Osman akionyesha uwezo wake Uwanja wa Taifa.

Hii ni kwa mara ya kwanza klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza kuzuru Afrika Mashariki na kucheza michezo ya kirafiki. Ujio wa kikosi hiki kinacho nolewa na kocha Ronald Koeman, pia ni sehemu ya maandalizi yao dhidi ya msimu ujao wa ligi ya EPL.

Akizungumza na Bongo5, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas, amesema kuwa ujio wa klabu hiyo si jambo la kufikirika na hivyo watanzania wajiandae kuishuhudia timu hiyo na wamejipanga kuhakikisha wana usaidia mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini.

Ikumbukwe kuwa Kampuni hii ya michezo ya kubashiri ya SportPesa, ilitangaza michuano ya SportPesa Super Cup itakayo fanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuwanzia tarehe 5 Juni nakumalizika 11 Juni 2017 na mshindi wa michuano hiyo kucheza na klabu ya nchini Uingereza ambayo kwa sasa inafahamika kuwa ni Everton.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents