Habari

Ujio Wa Tusker Lite Beer Una Neema Kwa Wapenda Muziki Wa R&B Na Neo Soul Tanzania.

Moja Ya tangazo la shoo ya Tusker lite Iliyofanyika Nairobi kenya iliyofanyika Tarehe 8 Mwezi wa Tisa 2012.

Hello party people, kampuni ya vinywaji vya bia na spirit ya East African Breweries, ambayo ni kampuni tanzu ya Serengeti Breweries, inaingiza kinywaji kipya katika soko la vinywaji Tanzania kwa kuleta aina mpya ya bia inayoitwa Tusker Lite ambayo moja ya kauli mbiu yake ni burudani laini ama nyororo kama bia yenyewe ilivyo.
Ujio wa kinywaji hiki, unaasilimia kubwa unakuja na aina ya burudani ya muziki inayoitwa “Neo Soul Music Experience” na kwa mujibu wa uchunguzi wetu, tayari nchi zote ambapo kinywaji hicho kimeingia, kama Kenya na Uganda imeambatana sambamba na aina hiyo ya burudani ya muziki.
Hii ni ishara nzuri kwa wale wote ambao wanapenda vinywaji visivyo na asilimia kubwa ya kilevi, lakini pia wapenda muziki wa taratibu na laini kwani wategemee burudani hiyo. Hatuna hakika lini hasa mpango huo utaanza, kakini speculations are rife from our side, tutegemee performance kutoka kwa wasanii kama kina Eric Benette, Johny Gill, Erykah Badu n.k.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents