Habari
Ujue mji ghali zaidi duniani, upo Africa
Mji mkuu wa Angola, Luanda, umechukua nafasi ya kwanza kama mji ghali zaidi duniani, huku mji wa Hong Kong ukishika nafasi ya pili.
Takwimu hizi zimetolewa na shirika la Mercer ambalo lilifanya utafiti. Katika takwimu hizo miji ya Tokyo, Zurich na Singapore pia nayo inachukua nafasi tano za kwanza. Mji wa London ulishuka hadi nafasi ya 30 hasa kutokana na kushuka kwa thamani ya paundi.
Utafiti huo wa kila mwaka huangazia masuala kadha kando na gharama ya kukodi nyumba. Utafiti huo huangazia gharama ya vitu 200 kwa kila mji, ikiwemo nyumba, usafiri, mavazi, chakula na burudani.
By Peter Akaro