Uncategorized

Ujumbe aliotumiwa Samatta na timu yake ya Genk kabla ya mchezo, Balozi wa Uingereza Tanzania nae aliipongeza Stars (+ Video)

Taifa Stars imefanikiwa kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kwa mara ya pili ikiwa ni maka 39 imepita tangu iingie kwenye michuano hiyo. Taifa Stars imefuzu kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Uganda, ambapo Matokeo mengine Lesotho imetoa sare ya 0-0 dhidi ya Cape Verde.

Goli la kwanza la stars lilifungwa na mshambuliaji Simon Msuva baada ya kupokea pasi kutoka kwa John Bocco. Mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 1-0.

Dakika tano baada ya kipindi cha pili kuanza, Stars walipata penati baada ya mpira uliopigwa na nahodha Mbwana Samatta kutua kwenye mkono wa mlinzi wa Uganda Cranes Kirizistom Ntambi kwenye eneo la hatari.

Magoli yote ya Taifa Stars dhidi ya Uganda.

Mkwaju wa penati hiyo ulisukumwa nyavuni na mlinzi Erasto Nyoni na kuiandikia Stars bao la pili.

Lakini pia timu ya mshambuliaji na nahodha wa taifa stars Mbwana Ally Samatta alitumiwa ujumbe huu na timu yake ya Genk kutoka nchini Ubelgiji.

Ushindi mnono kwa Stars ulihitimishwa katika dakika ya 57 mara baada ya beki Agrey Morris kufungwa kwa ustadi goli la kichwa akiunganisha krosi maridhawa iliyochongwa na John Bocco.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cook naye ametuma saqlamu zake za hongera kwa ushindi huo uliosubiriwa kwa miaka 39.

Kufuzu kwa Stars kunakamilisha moja ya historia kubwa ya mafanikio ya mpira katika kanda ya Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mataifa manne ya ukanda huo yamefuzu kuelekea Misri.

Polisi alivyoshindwa kujizuia na kumkumbatia kocha

Uganda wao walitangulia kufuzu mwezi Novemba 2018, na michuano ya mwaka huu itakuwa ya saba kwa taifa hilo kushiriki.

watu walivyovunja geti la uwanjani

Kenya ilikuwa ya pili kwa kufuzu katika ukanda huu kwa kufanya hivyo Disimba 2018., na wataenda Misri ikiwa ni mara yao ya sita kushiriki michuano hiyo.

Wachezaji wa taifa stars walivyotoa shukurani zao na maneno ya makocha wote

Burundi wao walifuzu siku moja kabla ya Tanzania kwa kutoka sare na Gabon. Hii ni mara ya kwanza kwa taifa hilo kushiriki michuano ya AFCON.

Ujumbe wa Twitter wa @Tanfootball: Mataifa yaliyofuzu Afcon 2019

Kwa ujumla, michuano ya mwaka huu yatashirikisha mataifa 24, ikiwa ni ongezeko la timu 8 kutoka awali ambapo zilikuwa zikishiriki timu 16.

By Ally Juma.



Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents