Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Ujumbe mzito wa JB kwa Bongo Movie

Msanii wa Filamu Bongo, JB amewataka wasanii wenzake kupenda kuweka vitu ambavyo vina uhusiano wa moja kwa moja sanaa yao katika mitandao yao ya kijamii na kupunguza mambo ambayo hayachangii kutangaza kazi zao.

Muigizaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa ukiangalia akaunti za wasanii wengi wa filamu kwa mwezi mzima anaweza asiposti kitu chochote kinachohusiana na filamu lakini wakumbuke kuwa filamu ndio iliyowafanya wajulikane.

“Watu wanawafahamu kwa sababu ya movie tusijisahau walau kwa wiki mara mbili, mimi nimepunguza sana kuposti mipira, ni movie tu na nimeacha kuwa-follow watu wasio husika na movie hata mke wangu” ameeleza JB.

Ameongeza kuwa si lazima wafanye kama yeye ila ni vema kubadilika na kuamka kwa ajili ya kutangaza kazi zao na si vinginevyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW