Burudani

Ujumbe wa Cheed na Killy kwa Alikiba baada ya kutambulishwa Konde Gang na harmonize

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva ambao walikuwa chini ya lebo ya @officialalikiba @kingsmusicrecords ambao ni @officialcheed na @officialkilly_tz wametambulishwa rasmi kwenye lebo ya @kondegang iliyopo chini ya @harmonize_tz

kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram, wasanii hao wapya wa Konde Gang wametanagza kujiunga na lebo hiyo  huku wakimshukuru boss wao wa zamani Alikiba kwa kuwaonyesha njia na kuwaamini kufanya nao kazi.

ameandika Cheed na Killy kuwa :-

Habari Za Muda huu Ndugu Zangu …!!! Nianze Kwa Kuwashukuru Nyinyi Wote ambao Mmekuwa Na Mchango Mkubwa Sanaa Katika Safari Yangu Ya Mziki..!!! Mmekuwa Namimi Bega Kwa Bega Ninapo Nashukuru Sana Kwakweli Upendo wenu Wadhati Na Unamaanisha.. Kilakitu Kwangu ….!!!! Shukrani Za Dhati Zimuendee Kaka Yangu Kipenzi AllyKiba Natambua..!! Na Nitaendelea Kuuheshimu Mchango Wako Milele Yote Ulijitoa Kuhakikisha Watanzania Wananifahamu Kwa Kiasi Mpaka Pale Mungu Alipo Tuamuru Kupitia Njia Nyingine Katika Safari Hii Ya Utafutaji Wa Riziki. Leo Nipo Mbele Yenu Zaidi ni Kuwashuku Kwa Kuwa Sambamba Nami Lakini Pia Kuwataarifu Rasmi kwamba Kijana Wako Nimejiunga Na Kampuni Ya Uzalishaji Na Usimamizi Wa Muziki Tanzania KONDE MUSIC WORLDWIDE @KONDEGANG hii ni faraja Kubwa Kwangu na Sio Faraja Tuu bali Nitumaini Jipya kama Kijana wa Kitanzania Kupata Nafasi Ya Kufanya Kazi kwa Ukaribu na Wasanii Wenzangu @HARMONIZE_TZ & @IBRAAH_TZ @Youngskells Nawengine Natambua Kuna Wengi hata Wenye Kipaji Kunizidi Wangetamani Kuwepo Hapa Lakini Naamini Kilakitu Huja Kwa Wakati…!! Naamini Kwa Pamoja Tutashirikiana Ili kuzitunza Familia Zetu Masikini Nimalize kwa Kushukuru Uongozi Wa KONDE MUSIC WORLDWIDE Kwa Nafasi hii Ya Peke pia Niwaombe Ndugu Zangu Muendelee Kutuunga Mkono Na Mungu atawabariki Sana …!!! #KONDEGANG4EVERYBODY

 

Cheed na Killy walijitoa Kings Music mwezi Aprili, hivyo wataungana na wasanii kama Ibrah Tz, Young Skales kwenye lebo ya Konde Gang ambayo inasimamiwa na Harmonize.

https://www.instagram.com/p/CE2JonxlSvc/

https://www.instagram.com/p/CE2KsQcFD8d/

https://www.youtube.com/watch?v=HwctESjdeFE

https://www.youtube.com/watch?v=lgMjkpAamsQ

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents