Burudani

Ujumbe wa Jaguar baada ya Uhuru Kenyatta kutangazwa Rais wa Kenya

By  | Msanii Jaguar wa Kenya na pia Mbunge wa jimbo la Starehe County ya mjini Nairobi kupitia muungano wa chama cha Jubilee, amempongeza Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena katika kiti cha Urais katika uchaguzi wa marudio ambao umefanyika wiki iliyopita.

Kupitia mtandao wa Twitter, Jaguar ameandika, “Congratulations @UKenyatta on your reelection. I thank all who voted and equally expressed their democratic right. Let’s maintain peace.”

Rais Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo (IEBC), Wafula Chebukati kupata kura 7,483,895 sawa na asilimia 98, mpinzani wake Raila Odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa naasilimia 0.96.

Jumla ya wananchi 7,616,217 walipiga kura katika uchaguzi huo kati ya watu milioni 19.6 waliojiandikisha kupiga kura.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments