Michezo

Ujumbe wa Klopp kwa Van Dijk baada ya kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka akiwashinda mastaa hawa wakubwa ‘Wewe ni mwanaume’

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amemtumia ujumbe beki wake wa kati, Virgil van Dijk baada ya hapo jana usiku siku ya Jumapili kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa PFA.

Image result for klopp and van dijk

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Netherlands ametwaa tuzo hiyo msimu huu wa mwaka 2018/19 baada ya mwaka jana kuchukuliwa na nyota mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah katika sherehe zilizofanyika jijini London.

Hata hivyo, Van Dijk alikutana na changamoto kutoka kwa wachezaji wenzake, Sadio Mane, Sergio Aguero, Bernardo Silva, Raheem Sterling, na Eden Hazard katika kuwania tuzo hiyo.

Klopp, alimsajili Van Dijk kutoka kwenye klabu ya Southampton mwezi Januari mwaka 2018 na kufanikiwa kuitumikia Liverpool kwa mafanikio makubwa.

“Najivunia kwa mara ya pili nazungumzia wachezaji bora ambao wameshinda taji hili kwa misimu hii,” amesema  Klopp.

“Ni vigumu kufiria pale ukirudi nyuma alivyokuwa, na ilikuwa ngumu kwa kila mtu kufahamu yeye ni aina gani ya mchezaji na kile alichojaaliwa kuwa nacho kwenye mwili wake.”

“Lakini kwa sasa dunia nzima inamfahamu najisikia furaha naniaweza kuwa na mchango kidogo kwenye sehemu yake ya mafanikio.”

“Tangu mwanzo nilikuwa nimevutiwa mno kuhusu nafasi aliyopata na kufanyanaye kazi pamoja, sasa wewe ni mwanaume angalau kwa msimu huu.”

Kwenye tuzo hizo za PFA, juma la wachezaji wa nne wa Liverpool wametajwa kwenye kikosi cha PFA Premier League msimu wa mwaka 2018-19, ambao ni  Trent Alexander-Arnold, Mane, Andy Robertson na Van Dijk .

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents