Michezo

Ujumbe wa mchezaji huyu wa Manchester United akimdhihaki Lukaku baada ya kutolewa UEFA, waleta gumzo mitandaoni

Ujumbe wa mchezaji huyu wa Manchester United akimdhihaki Lukaku baada ya kutolewa UEFA, waleta gumzo mitandaoni

Ujumbe alioupost tarehe 21/10/2019 aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Lukaku alipost akionyesha kufurahia kucheza UEFA baada ya kuondoka Manchester United na kuhamia Inter Milan kwani Man United haikupata nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA kutokana na kutokufanya vizuri katika ligi kuu nchini Uingereza hivyo kucheza michuano ya UEFA Europe League.

Lukaku alifanya hivyo na kutafsiriwa kuwa alikuwa akiwathihaki Man United kwa kuwa wao hawakuwepo kwenye hiyo michuano inayoamikia kuwa ndio michuano mikubwa zaidi barani Ulya na kila mchzaji hata klabu inatamani kucheza.

Usiku wa kuamkia leo tarehe 11/12/2019 baada ya Inter Milan kutupwa nje ya michuano hiyo na kupata nafasi ya kucheza UEFA Europe league , kwani kwenye kundi lao zimefanikiwa kupita timu mbili tu ambazo ni Barcelona kutoka nchini Uhispania na Borusia Dortmund kutoka nchini Ujerumani huku Inter Milan na Slavia Praha kutupwa nje baada ya kupoteza michezo yao ya jana.

Inter Milan ambayo ilikuwa inacheza na Barcelona ilifungwa 22-1 ikiwa nyumbani kwao huku Slavia Praha nao wakifungwa 2-1 na Dortmund wakiwa ugenini.

Sasa baada ya Inter Milan kutupwa nje ya michuano hiyo na kwenda kushiriki UEFA Europa League beki wa Man United Luke Shaw ame-Retweet post hiyo na kumwambia karibu tena UEFA Europe league, kitendo kinachotafsriwa kuwa kumdhihaki kwa timu yao kutolewa kwenye michuano hiyo,

https://twitter.com/footblab/status/1204562000233324544

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents