Burudani

Ujumbe wa Rayvanny kwa Diamond, ‘Hakuna anayefanikiwa akakosa maadui’

Msanii kutoka WCB, Rayvanny amefunguka mambo kadhaa kwa kile anachopitia Diamond kwa sasa katika muziki wake.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa hakuna anayefanikiwa akakosa maadui na ndicho kinachotokea kwa Diamond sasa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rayvanny ameandika;

Kuna Vitu Pengine Unaweza Ukawa Unapatia Au Vingine Unakosea Sitaki Kuongelea Hilo Sababu we nawe Ni Binadamu. ILA KWENYE KUSEMA UKWELI NITASEMA!!!! Si kwa Sababu wewe Ni boss Wangu Hapana!!! Ila Mara Nyingi Thamani Ya mtu Na Umuhimu Wa Mtu wengi Wanaujua Akishaondoka…. MZIKI NI KAZI NA NI AJIRA Namaanisha Kuna Familia Nyingi Zinaishi kupitia Huu huu mziki.

DIAMOND KATIKA WASANII WOOOTE Umekua chachu Ya Kuongeza Thamani Ya Muziki Nakupitia wewe naamini Wengi Wanafanikiwa…. KUJITOA KWAKO, KUAMINI KATIKA UMOJA NA PIA KUTHUBUTU Ndiko kunafanya Unafanikiwa…. USHAAMBIWA HUJUI KUIMBA ila ukaimba ukafanikiwa… USHAAMBIWA UNAVIMBA UNAIGIZA MAISHA Lakini sasa Unayaishi hayo Maisha… Hakuna Anaefanikiwa Akakosa maadui ndivyo Dunia Ilivyo ..

MIMI ULINISAIDIA ULIJUA SHIDA ZANGU Naamini Mungu Alikutumia wewe Ukawe Mkombozi Wangu ……. KWAIO KUMBUKA ( ILI MBEGU IOTE LAZIMA IOZE ) SINA MUDA KUMSEMA MTU ILA NAKUPA MOYO FANYA KAZI SIMBA……. kama Wewe Unaamini Katika Upendo Na sio Chuki, Vita Na Matusi JUS COMMENT ( LOVE )

Kwa siku za hivi karibuni Diamond amekuwa kwenye drama kibao kufuatia kutofautina na baadhi ya vyombo habari kitu kilichopelekea kutochezwa kwa nyimbo zake katika vyombo hivyo, pia kufungiwa kwa nyimbo zake mbili ‘Waka na Hallelujah’ ni moja ya mambo ambayo hayajakaa vizuri kwa upande wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents