Habari

Ujuzi wako ni upi? Ikitokea umepoteza kazi uliyonayo, nini unaweza kufanya?

Je wewe ndo unayestahili kuwa kwenye nafasi hiyo? Kitu gani ulichonacho kinakufanya uonekane wa kipekee kwenye kazi yako? Je tokea umechukua nafasi hiyo jambo gani unajivunia wewe binafsi au unahisi kufanikiwa kitaaluma? Kama unashindwa kujibu maswali hayo nina wasiwasi na ujuzi wako na umefikaje hapo?

5367330322_6e9cd18b65_b

Mara nyingi nimekuwa nikitegemea cheti changu kupata kazi fulani fulani na nikifikiri ninastahili.  Mara nyingine nikitolea mfano wa chuo nilichosoma na umaarufu wake. lakini cha ajabu kazi ninayofanya haina tofauti sana na mtu aliyeishia kidato cha sita zaidi ya vikao vingi na kusaini nyaraka mbalimbali. Kazi yangu ni nini hasa? Je taaluma yangu inahusika vipi hapa? au kwasababu ya cheti changu, je mimi ni bora kuliko mfagiaji?

Naendelea kufikiri, tumaini langu liko wapi endapo kazi hii nikisimamishwa au kufukuzwa, je nitasimama vipi katika biashara zangu au kupata kazi nyingine? Ujuzi wangu ni upi hasa? Je ninapofikiri nina thamani ya mshahara wa ngazi fulani, nikianzisha kampuni je nitamlipa mtu mshahara kama huu kwa namna ninavyofanya kazi? Ninajaribu kufikiri tu.

Hebu turudi kwenye ujuzi wako ni upi? Je kampuni au ofisi hiyo wanakulipa kwa sababu ya nini hasa? Watu wengi tumekuwa na vyeti lakini hatuna ujuzi fulani ambao utatufanya tuweze kuishi hata kama ukifukuzwa kazi. Je ujuzi wako unaweza kuwa biashara? Au wewe ni wakusaini nyaraka huna jipya, huna mbele wala nyuma, ukiondolewa hapo unatafuta mchawi ni nani?

Naomba kukukumbusha anza kupunguza mawazo na chukua hatua, ujuzi ulionao kama siku moja hauwezi kukulipa nje ya ajira fikiri mara mbili. Inamaanisha wewe ni mtu wa kuajiriwa tu mpaka unastaafu, je baada ya hapo utakuwa unafanya nini? Fikiri sasa ili usije shangaaa miaka kumi au ishirini ijayo, mambo mengi yatakuwa yamebadirika kama tutakuwa hai. Teknolojia itakuwa imeenda mbali, hatutakuwa na watu wa kutunza mafaili kama ofisi nyingi za serikali, kutakuwa na watu wanaofanya kazi kwa ujuzi wao kama huna maisha yatakuwa magumu sana kwako. Fikiria mara mbili na uchukue hatua.

Kama una mpango wa kufanya biashara na taaluma yako si biashara, unatakiwa kujifunza biashara kwani ushindani ni mkubwa na mambo hayataenda vile unavyofikiri. Kwa kila kitu ambacho unampango wa kukifanya kwenye taaluma yako au Biashara yako unatakiwa ukijue kiundani ili upate matokeo bora zaidi. Bila Kusahau ujuzi wako ni Upi? Na unafanya nini?

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents