Habari

Ukilalamika kuwa wewe ni mfupi, fikiria mara mbili kuhusu wasichana hawa warefu zaidi duniani

Ukianza kulalamika kuhusu wewe kuwa mfupi, huwezi kushika dali au kubadilisha balbu (taa), kuna msichana mwenye chini ya miaka 18 na ana urefu wa futi 9 na inchi 9, anayepata shida kuingia kwenye gari. 

o-MY-GIANT-LIFE-570-4

Binti huyu alikuwa akihojiwa kwenye kipindi kinachorushwa kwenye runinga ya TLC huko majuu kuhusu wanawake wenye futi 6.6 wanavyopata shida na maisha tu ya kawaida kama kuosha na kuviweka vyombo vya ndani kwenye droo za makabati, au kwenda dukani ama kwenye maduka makubwa ya kisasa yaani super market.

Binti mmoja wa miaka 17, Nancy ana futi 6.9 ambao unampa shida kupata gauni la kutoka nalo na ana wasiwasi kama atapata mwenza kwenye sherehe inayokuja wa kutoka naye. Na ugumu ambao anaupata ni katika harakati za kujifunza kuendesha gari ambapo imekuwa vigumu kupata gari la kumtosha miguu yake kukaa vizuri.

Changamoto nyingine iko kwenye nyumba wanazoishi, zinatakiwa ziwe na dali lenye urefu wa kutowasumbua. Vilevile vitanda si vya kawaida kama vya kwetu 6 kwa 6, kitanda cha 6 kwa 6  hakitoshi hivyo lazima urefu uongezeke na godoro hivyo hivyo kuagizwa maalumu kwaajili yake.

Vile vile shida anayopata Nancy haina tofauti na anayopata mwigizaji na mcheza mieleka wa kike Lindsay ambaye naye ana futi 6.9. Lindsay inapata sana shida akisafiri kwenye ndege hasa anapotakiwa kwenye chooni, ingawa watu wengi humwona kama ana furaha anapopita mtaani au kwenye maeneo ya michezo kwakuwa hakuna wa kumzuia mbele yake.

Watu hupenda kumtania kwa kumwita “Mtoto wa Twiga”.

o-MY-GIANT-LIFE-570

Faida ambayo anaipata Haleign mwenye futi 6.7 ni kwa yeye kujiunga kwenye timu ya mchezo wa mikono ‘volleyball’ hivyo anaweza kusafiri sehemu nyingi duniani kutokana na kutegemewa sana na timu yake kwa sababu ya urefu wake. Changamoto imekuwa ni kupata mwenza, ingawa anajitahidi kutafuta.

o-MY-GIANT-LIFE-570-2 o-MY-GIANT-LIFE-570-3

Haleigh, mwenye umri wa miaka 23, anataka kuolewa lakini hana uhakika kama baba yake atamkubali mchumba wake ambaye ana umbo dogo na ana urefu wa futi 5.6 ambayo ni changamoto kwani hata kumpiga busu inabidi kijana huyo asimame kwenye ngazi ya mrango ili aweze kumfikia mchumba wake.

Pamoja na changamoto hiyo lakini wanapendana na wako tayari kuendelea na maisha ya ndoa.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents