Burudani

Ukimya unapoteza wasanii wengi – Chege

Msanii Chege amedai ukimya bila kutoa ngoma ni moja ya sababu kupotea kwa wasanii wengi.

Akizungumza na Bongo5 Chege amesema licha ya hilo hata utoaji wa ngoma usiokuwa na mpangilio nao unachagia hilo na ndio sababu ya kuzipa muda ngoma zake katika ya miezi miwili.

“Watu wanapenda kusikiliza ngoma mpya, game imebadilika kwa sababu mfumo wa zamani mtu ulikuwa unajipangia kwa mwaka natoa ngoma mbili au tatu sasa hivi haiwezekani, ukiwa na hamu ya kupotea basi fanya hivyo,” amesema Chege.

“Ukimya unapoteza wasanii wengi na kutoa ngoma ile bampa to bampa, inatakiwa unajiangalia nimetoa ngoma leo nitoe tena muda gani, miezi miwili inakuwa ni standard nzuri na ndio kitu ambacho mimi nakifanya,” ameongeza.

Kuanzia February hadi August mwaka huu Chege ametoa ngoma nne ambazo ni Kelele za Chura, Go Down, Najiuliza na Run Down.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents